Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

KAONGEZENI UPENDO KWA WAGONJWA ONDOENI MALALAMIKO KWA WAHITAJI.

Posted on: May 15th, 2024Na WAF-Mbeya


Katibu Tawala wa mkoa wa Mbeya Rodrick Mpogolo amewataka madaktari Bingwa wa Rais Samia kufanya kazi kwa weledi na upendo kwa wagonjwa Pamoja na kuondoa malalamiko kwa wahitaji ikiwa ndio lengo la Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassani kupitia wizara ya Afya na TAMISEMI.


Katibu Tawala Mpogolo ameyasema hayo wakati akiwapokea Madaktari Bingwa wa Dkt Samia kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mhe Juma Homera baada ya Madaktari kuwasili mkoani Mbeya kwa ajili ya kuwadumia wanaachi katika Hospitali za Halmashauri saba zilizopo mkoa wa Mbeya,


Hata hivyo  Mpogolo amewaasa Madaktari Bingwa kwenda kufanya kazi kwa kujituma zaidi wakitanguliza upendo na kuwajali wagojwa ili kutimiza lengo la Mhe. Rais na Wizara ya Afya kwa wananchi. 


“Sisi kama mkoa tumejipanga kuhakikisha wananchi wanapata huduma nzuri kama mhe. Rais alivyokusudia kuona wananchi wanasogezewa huduma za kibingwa karibu zaidi”. Amesema Mpogolo


Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dkt Elizabeth Mnyema ametoa shukrani kwa Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwasogezea wananchi karibu huduma za kibingwa katika ngazi ya Hospitali za Halmashauri ambapo kila Hospitali itakuwa na Madaktari watano 


“Matarajio yetu makubwa  ni kuwafikia wananchi katika kutoa huduma  za kibingwa  pia madaktari wetu waliopo katika maeneo yetu ni kupata ujuzi kwa ajili ya kuboresha huduma kwa wananchi mara baada ya hili zoezi kuisha”. Amesema Dkt. Elizabeth


Aidha ameendelea kutoa wito kwa wananchi waweze kufika katika kwenye Hospitali zote za Halmashauri ili waweze kupata Huduma za kibingwa ambazo zinesogezwa na mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kupitia uratibu wa wizara ya Afya na TAMISEMI.