Customer Feedback Centre

Ministry of Health

WAGONJWA WANNE WALIOPANDIKIZWA FIGO MLONGANZILA WARUHUSIWA

Posted on: October 12th, 2023


Na WAF - Dar es salaam


Hospitali ya Taifa Muhimbili, Mloganzila kwa mara nyingine imepata mafaniko makubwa kwa kushirikiana na Korea International Foundational for Health Care na Africa Future Foundation kwa kufanya upandikizaji wa figo kwa wagonjwa wanne ambao figo zao zimeshindwa kufanya kazi.


Mkurugenzi mtendaji wa Hospital ya Muhimbili Prof. Mohamed Janabi ameyasema hayo Oktoba 13, 2023 baada ya kutoa ruhusa kwa wagonjwa Wanne waliopandikizwa Figo katika Hospitali hiyio.


“Upandikizaji huo ni wa kipekee hapa nchini kwa kuwa umetumia utaalamu wa kisasa ambapo figo imevunwa kutoka kwa mchangiaji kwa kutumia njia ya matundu madogo (Hand assisted Laparoscopic Donor Nephrectomy).” Amesema Prof. Janabi


Akizungumzia upandikizaji huo katika hafla ya kuwaaga waliopandikizwa figo, Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Mohamed Janabi amesema utaalamu uliotumika kuvuna figo kwa kutumia matundu unafanyika Mloganzila pekee kwa Hospitali za Umma nchini na Afrika Mashariki na Kati.


“Kwa kutumia njia ya matundu mchangiaji anakuwa na kovu dogo, anakaa hospitali kwa muda mfupi takribaini siku mbili hadi tatu kitu ambacho kinasaidia kupunguza gharama kwa hospitali na mchangiaji pia” amebainisha Prof. Janabi.


Aidha, Prof. Janabi ameishukuru Serikali kwa uwekezaji ilioufanya ambapo amefafanua kuwa Mloganzila kuna vyumba vya upasuaji vya kisasa na vyumba vya uangalizi maalumu vyenye mashine na vifaa vya kisasa na pia kuna wataalamu bingwa na bobezi waliojengewa uwezo na Serikali katika nyanja tofauti tofauti.