Customer Feedback Centre

Ministry of Health

WANAHABARI WATAKIWA KUWA MABALOZI ELIMU YA AFYA MABUSHA, MATENDE

Posted on: January 7th, 2026

Na WAF - Dar es Salaam

Serikali kupitia Wizara ya Afya imewataka Wanahabari kuwa sehemu ya Mabalozi utoaji wa Elimu ya Afya kuhusu Mabusha na Matende ugonjwa ambao umekuwa ukiwakabili watu kutokana na kuwa elimu duni juu ya ugonjwa huo.

Hayo yamebainishwa leo, Januari 06, 2026 na Mratibu wa Matende na Mabusha Kitaifa, Mpango wa Taifa wa Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele kutoka Wizara ya Afya, Dkt.Bulinja Anthony wakati wa utoaji wa Semina kwa Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam.

"Wanahabari ni nguzo muhimu sana katika utoaji wa elimu ya afya kuhusu magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ikiwemo Mabusha na Matende"amesema.

Aidha, Dkt. Antony amesema kambi ya upasuaji wa Mabusha Mkoa wa Dar es Salaam imeanza tangu tarehe 05, Januari, 2026 hadi tarehe 30, Januari, 2026, huku akiwataka wananchi kuchangamkia huduma hiyo.

"Katika kambi hii tumelenga kuwafikia wananchi zaidi ya mia tano wenye tatizo la Mabusha na tutafanya katika Kituo cha Afya Kinondoni na Kituo cha Afya Kilakala kilichopo Temeke"amesema.

Kwa upande wake Mratibu wa Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Dkt.Irene Haule amesema Faida ya Kambi hiyo ni mwananchi kufanyiwa uchunguzi na madaktari Bingwa

Kwa upande wao baadhi ya Waandishi wa Habari waliopatiwa Mafunzo hayo wamesema watakuwa mabalozi wa kuelimisha jamii namna ya kujikinga na Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele.