Customer Feedback Centre

Ministry of Health

TANZANIA NA MOROCCO WAKUBALIANA MASHIRIKIANO KATIKA HUDUMA ZA AFYA

Posted on: May 21st, 2025

Na WAF - Geneva, Uswisi

Ziara ya kikazi ya Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama akiwa ameambatana na Waziri wa Afya (Zanzibar) Mhe. Nassor Mazrui nchini Uswisi imeendelea kuzaa matunda kwa wadau mbalimbali wakiwemo Mawaziri kuiunga mkono Tanzania katika masuala ya afya.

Katika kikao chao baina ya Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama na Waziri wa Afya wa Morocco Mhe. Amine Tehraoui pamoja na mambo mengine wamekubaliana kushirikiana na kuboresha huduma za afya ya uzazi mama na mtoto pamoja na uzalishaji wa bidhaa za dawa ikiwemo chanjo.

"Nakushukuru sana kwa kukutana nasi, na hakika tukiendelea kushirikiana kwa pamoja tutaweza kuendelea kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi lakini pia tutaweza kujitegemea katika kujizalishia bidhaa za dawa wenyewe ndani ya nchi bila kuagiza nje," amesema Waziri Mhagama