Customer Feedback Centre

Ministry of Health

NAIBU KATIBU MKUU ATOA WITO KWA JAMII KUJIUNGA NA MFUKO WA BIMA YA AFYA KWA WOTE.

Posted on: February 8th, 2024

Na WAF - Rukwa


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe Ametoa wito kwa wananchi kujiunga na mfuko wa taifa wa Bima ya afya kwa wote ili kuchangiana matibabu kwa na wawezesha wanajamii kupata huduma bora za Afya kwa urahisi zaidi.Dkt. Magembe amesema hayo Februari, 8 2024 wakati wa ziara ya Kikazi mkoani Rukwa Wilayani Sumbawanga, yenye lengo la kukagua utendaji kazi wa watumishi katika sekta ya afya.


Dkt. Mageme amesema kutoka na hali za maisha za wananchi wengi wa Tanzania, kumudu gharama za matibabu wakati mwingine huwa ni chamgamoto ndio maana Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amesaidia sheria ya Bima ya afya kwa wote ili kuweza kuwawezesha wananchi kupata huduma za afya kwa wepesi na haraka zaidi.“Hali ya maisha ni ngumu kwa sote, na kuna muda huwenda ikawa ni changamoto kumudu gharama za matibabu aidha kwako au ndugu yako, hivyo kujiunga na Bima ya afya kwa wote itakwenda kuleta unafuu katika hali ya maisha na kupata matibabu yoyote yanakusumbua.” amesema Dkt. Magembe.


Aidha, Dkt. Magembe ameongeza kuwa Mhe. Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uwekezaji mkubwa katika Sekta ya Afya ya kusogeza na kuhakikisha vifaa tiba vya kisasa na dawa zinapatikana katika Hospital na vituo vyote vya kutolea huduma za Afya nchini ili kuwawezesha wananchi kupata huduma za afya kwa ukaribu zaidi.“Uwekezaji wote uliofanywa na Dkt. Samia Suluhu Samia ni kwajili yenu watanzania wenzangu hivyo ni jambo la kujivunia, hiyo kama kuna uzembe au hampatiwi huduma inayoendana na mabadiliko haya ya maendeleo yaliyofanywa basi mtoe taarifa sababu mawasiliano yetu yapo yamebandikwa hospitali zote nchini” amesema Dkt. Magembe.


MWISHO.