Customer Feedback Centre

Ministry of Health

MWENGE WA UHURU WAZINDUA JENGO LA UZAZI SUMBAWANGA

Posted on: September 30th, 2025

NA WAF – RUKWA

Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Mhe. Nyakia Ally Chirukile, amezindua rasmi jengo jipya la uzazi katika wilaya hiyo, hatua inayolenga kuboresha huduma za afya ya uzazi kwa wananchi.

Akizindua jengo hilo leo, Septemba 29, 2025, Mhe. Chirukile amesisitiza umuhimu wa jengo hili katika kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma bora za uzazi kwa urahisi.

Mhe. Chirukile amesema uzinduzi huu unaashiria jitihada za Serikali za kuimarisha huduma za afya za msingi na kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma bora karibu yake.

“Nitoe wito kwa wananchi kutoa ushirikiano ili kuhakikisha jengo hili linatumika ipasavyo na linatoa manufaa kwao,” amesema Mhe. Chirukile.

Aidha, Mhe. Chirukile amewakaribisha madaktari bingwa waliowasili mkoani Rukwa kwa ajili ya kutoa huduma za kibingwa katika halmashauri zote za mkoa huo.

Kwa upande wake, Kiongozi wa Mbio za Mwenge, Bw. Ismail Ali Ussi, amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha huduma za afya zinasogezwa karibu na wananchi.

Bw. Ussi amewahimiza madaktari watakaotoa huduma katika kituo hicho kuzingatia mwongozo wa utoaji huduma ili wananchi waweze kunufaika na fedha zilizotolewa na Serikali.