Maoni Ya Wateja

WODI 75 ZA WAGONJWA WA DHARURA KUJENGWA KATIKA HALMASHAURI 75 NCHINI

Posted on: August 12th, 2022

Na Englibert Kayombo , WAF – Mafinga, Iringa.

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa Serikali inajenga wodi za wagonjwa wa dharura 75 katika Halmashauri za Wilaya 75 nchini

Waziri Ummy amesema hayo alipokuwa akizungumza na wakazi wa Wilaya ya Mafinga, Iringa mara baada ya kupata nafasi ya kuzungumza na wananchi kwenye Ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa Mafinga Mkoani Iringa.

“Wodi za wagonjwa wa dharura zilikuwa kwenye baadhi ya Hospitali chache za Mikoa, za Kanda na Taifa, chini ya Rais Samia Suluhu Hassan tunajenga wodi za wagonjwa wa dharura 75, katika Halmashauri 75 ikiwemo Halmashauri ya Mafinga” amesema Waziri Ummy Mwalimu.