Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

WIZARA YA AFYA KUSHIRIKIANA NA JICA KUIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA UZAZI, MAMA NA MTOTO

Posted on: December 18th, 2023

Na WAF, Dar es Salaam

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. John Jingu amekutana na Shirika la Kimataifa la Ushirikiano la Japan JICA kujadili namna ya kuboresha huduma bora za afya kupitia mradi wa kuimarisha Huduma ya Afya na matunzo ya uzazi na watoto wachanga.


Hayo yanajiri leo Disemba 18, 2023 katika kikao kilichofanyika katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya zilizopo jijini Dar es salaam ambapo pia Dkt. Jingu aliwashauri katika kuboresha huduma za afya 


Aidha Dkt. Jingu amelishauri shirika hilo katika kuboresha huduma za afya ni vyema kuboresha mafunzo kwa wahudumu wa afya katika utoaji bora wa Huduma bora ili iweze kuimarisha Huduma za afya katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini.


“Tunatakiwa kuwajengea mafunzo wahudumu wetu wa afya katika maeneo tofauti tofauti ili kuweza kuimarisha Huduma hii ya mama mjamzito na watoto wachanga ili kuendelea kuboresha Huduma bora kwa mama na mtoto”. Amesema Dkt. jingu


Pia, Dkt. Jingu amelishauri shirika hilo katika kuendelea kuboresha miundombinu ya mama wajawazito na watoto wachanga na kujenga miundombinu katika maeneo ambayo hayana ikiwemo kitengo cha utunzaji mkubwa wa watoto wachanga (NICU) na jengo la Uzazi.


Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Tiba anaesimamia Hospitali za Rufaa za Mikoa Dkt. Caroline Damian amesema Serikali kupitia Wizara ya Afya imedhamiria kuwa na vituo sita vya ubora wa Huduma za Afya ya Uzazi na Watoto Wachanga nchini.