WAUGUZI, WAKUNGA ZINGATIENI MAADILI YA KAZI ZENU
Posted on: March 19th, 2024
Na WAF, Dodoma
Serikali kupitia Idara ya huduma ya Uuguzi na Ukunga imewataka watumishi katika kada hizo kuzingatia maadili ya taaluma na uwajibikaji wa pamoja kwa watumishi hao.
Rai hiyo imetoewa Machi 19, 2024 na Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Uuguzi na Ukunga Bi. Ziada Sellah wakati wa siku ya pili ya kikao kazi cha tathimini ya utekelezaji wa utendaji kazi wa huduma za uuguzi na ukunga nchini.
“ili kuhakikisha huduma za uuguzi na ukunga zinaimarika ni vema kuzingatiwa kwa huduma staha na mawasiliano madhubuti ukikutana na mgonjwa, amesema Ziada na kuongeza
"hata kama dawa hakuna inategemea unaongea kwa Lugha gani kama utaweza kuwasiliana nae vizuri ina maana mgonjwa huyu hawezi kulalamika , hivyo niwahimize watoa huduma za afya kufuata miongozo, kanuni na sheria za uuguzi na ukunga “ amesisitiza Bi. Ziada.
Katika hatua nyingine amesema Wauguzi wanamchango mkubwa katika upatikanaji wa huduma za afya kwa wote kwani wao hutumia muda mwingi kukaa na mgonjwa.
“Wauguzi ndani ya 24, siku saba za wiki utawakuta katika eneo la kazi hii inamaana ya kuwa hawa ndio wanaleta matokeo makubwa katika sekta ya afya ambapo kwa sasa tunaweza kuona mfano wa chanjo iliyofikia asilimia 90, hiyo inatokana na kazi yao kubwa wanayofanya.
MWISHO.