Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

WATUMISHI WA WIZARA YA AFYA WAHAMIA KWENYE JENGO JIPYA, MTUMBA.

Posted on: July 21st, 2025

Na WAF DODOMA.


Watumishi wa Wizara ya Afya waliopo Makao Makuu ya Wizara leo Julai 21, 2025 wamehamia na kuanza rasmi kutoa huduma katika jengo jipya la Wizara ya Afya lililopo katika Mji wa Serikali Mtumba, Dodoma.


Hatua hiyo inajiri mara baada ya kukamilika kwa jengo hilo ambalo limegharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 26.6 na sasa litawawezesha Watumishi wote wa Wizara ya Afya makao makuu kufanya kazi katika eneo moja hivyo kuleta ufanisi zaidi wa huduma zinazotolewa.


Jengo hili lina mita za mraba 14,355 likijumuisha sakafu kumi (10) mbili zikiwa ni sakafu za ardhini (basement), jengo litakuwa na ofisi zaidi ya 188 pamoja na kumbi za mikutano 13.


Wananchi wote wenye uhitaji wa kupata huduma tunawakaribisha kufika katika ofisi hizi mpya katika muda wa saa za kazi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (07:30 am) mpaka saa tisa na nusu mchana (03:30 pm) Jumatatu mpaka Ijumaa.