Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

WATOA HUDUMA ZA AFYA KUPIMWA UTENDAJI KAZI WA UTOAJI WA HUDUMA BORA KWA WANANCHI

Posted on: August 12th, 2022

Serikali imedharimia kuboresha utoaji wa huduma bora za afya kwa wananchi na kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za matibabu hivyo watoa huduma za afya kupimwa utendaji kazi wao wa utoaji huduma bora kwa wananchi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu alipokuwa akizungumza na wakazi wa Wilaya ya Mafinga, Iringa mara baada ya kupata nafasi ya kuzungumza na wananchi kwenye Ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa Mafinga Mkoani Iringa.

“Mwelekeo wa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ni ubora wa huduma na sio bora huduma” amesema Waziri Ummy na kuendelea kusema kuwa watoa huduma za afya watapimwa kwa muda wa utoaji wa huduma za matibabu, vipimo na upatikanaji wa dawa, pamoja na utoaji wa huduma bora kwa wakina mama na Watoto.

“Nataka niwaahidi mbele ya Rais wangu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan tutahakikisha vifo vya wakina mama wajawazito pamoja na Watoto wachanga vinapungua na kuvimaliza kabisa” amesema Waziri Ummy.