Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

WATAALAMU WA HUDUMA ZA DHARURA ZA MAMA NA MTOTO WACHANGA WATAKIWA KUWEZESHA MATUMIZI BORA YA VIFAA

Posted on: December 8th, 2023


Wataalamu wa afya waliohudhuria Mafunzo elekezi ya huduma za dharura ya uzazi na Watoto wachanga (EmONC) wametakiwa kuwezesha vituo vya afya kuona umuhimu matumizi bora ya vifaa na kuanzisha huduma mpya ambazo zitawasaidia kuokoa Maisha ya mama na mtoto.


Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa huduma za mama na mtoto Dkt. Ahmad Makuwani wakati wa Mafunzo elekezi ya wataalamu wa (EmONC mentorship) Kampeni ya Mama Samia iliyofanyika Disemba 8, 2023 jijini Dodoma.


Dkt. Makuwani amesema kuwa Mafunzo hayo yawe chachu ya kuwafanya wataalamu hao kwenda kutumia ujuzi walionao katika kuboresha huduma za mama na mtoto ili kuendelea kuzuia vifo vya mama na mtoto.


Aidha Dkt. Makuwani amesema kuwa kupitia Mafunzo hayo wanatarajia kuona baadhi ya huduma zinafika mahala pake kwa kutumia njia za kujifunzia ambazo hazibadiliki katika Nyanja ya Mafunzo.


“Hizi steps of learning huwa hazibadiliki, hivyo tunatarajia kuona baadhi ya product zinafika mahali pake, ni muhimu mkaoneshe umuhimu wa matumizi ya vifaa na sio kukaa stoo”.


Aidha Dkt. Makuwani amewaasa wataalamu hao kutumia lugha zenye staha ili kuboresha huduma na si kutumia lugha za ukali kwani lengo la kampeni ni kujifunza na kuboresha huduma za mama na mtoto.