Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

WANAWAKE 228 WILAYA YA HANANG WASHEHEREKEA SIKU YA KUZALIWA KWA RAIS. DKT. SAMIA KWA KUFANYA UCHUNGUZI SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI.

Posted on: January 27th, 2024


Jumla ya wanawake 228 wa Mkoa wa Manyara wilaya ya Hanang wameadhimisha Siku ya Kuzaliwa kwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kufanya uchunguzi wa saratani ya Mlango wa Kizazi. 


Uchunguzi huo ulifanyika Januari 27, 2024 katika vituo vya kutolea huduma za Afya 40 katika mkoa wa Manyara.


Ambapo wanawake 3 wamegundulika kuwa na maambukizi ambapo mmoja alipewa rufaa ya kwenda katika Hospitali ya  Haydom