Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

WAHUDUMU WA AFYA NGAZI YA JAMII KUTOA ELIMU YA LISHE NA UZAZI WA MPANGO KWA WANANCHI

Posted on: April 5th, 2024Na WAF - Dodoma

Serikali kupitia Wizara ya Afya imebainisha mikakati ya uboreshaji wa afua za Lishe pamoja na Uzazi wa Mpango ikiwemo kuwatumia wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii kutoa elimu kwa wananchi.

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amebainisha hayo leo Aprili 5, 2024 kwenye kikao kifupi baina ya Mawaziri kutoka Wizara za Kisekta na ugeni kutoka nchini Uingereza ukiongozwa na Waziri wa Uingereza wa Maendeleo na Afrika Mhe. Andrew Mitchel.

“Mikakati hii ambayo tumeanza nayo ya utoaji wa elimu ya Lishe pamoja na Uzazi wa Mpango kwa wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii ili watumike kutoa elimu ya afua hizo kwa wananchi kwa kuwa wao ndio wapo karibu zaidi na wananchi.” Amesema Waziri Ummy

Miongoni mwa viongozi waliohudhuria katika kikao hicho ni pamoja na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Adolf Mkenda, Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania Mhe. David Concar pamoja na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. James Mdoe