Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

UWEKEZAJI KISAYANSI KUTATUA CHANGAMOTO SEKTA AFYA

Posted on: June 7th, 2024


Na WAF - Dar es Salaam 


Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. John Jingu amesema Serikali inaeendela kuwekeza upande wa Sayasi kwaajili ya kutatua changamoto za kijamii hasa zinazoboresha hali ya huduma za Sekta ya Afya nchini.


Dkt. Jingu ameyasema hayo Leo Juni 7, 2024 wakati wa hafla ya kuwapongeza wanafunzi Waliofanya Vizuri Zaidi Katika Masomo ya Sayansi (Baiolojia, Fizikia na Kemia) wa Kidato cha Nne na Sita kwa Mwaka 2021 na 2022 & inayoratibiwa na Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.


"Sayansi ni Duniani ya Leo na kesho, Mengi tunayoyaishi leo ni Matunda ya Sayansi, sayansi ndio inatupa majawabu ya mambo makubwa na changamoto zinazo itatiza jamii zetu, amesema Dkt. Jingu na kuongeza


"Kwa kuliona hilo ndio maana Serikali inaona ni muhimu sana kuendelea kuwekeza eneo la Sayansi ili kuwa na wanayasayansi mahiri ambao watajibu na kutatua maswala makubwa ambayo yanayotusumbua katika njanja zote." amesisitiza Dkt. Jingu 


Dkt. Jingu ametoa wito kwa wanafunzi hao kuendela kuziishi dhana na kanuni za Sayansi na ndoto zao kwani Sekta ya Afya bado inafursa zenye uhitaji wa watu wa kada hiyo. 


"Dunia na Ubinadamu kwa ujumla wake tunawategemea mje mtimize ndoto zenu na msaada katika Sekta ya Afya elimu yenu iwafanye mje na mbinu mpya za kutatua changamoto kwa sababu magonjwa kila siku yanazuka mapya, vimelea vinabadilika tabia nchi kwa kila nyanja tutawategemea nyie wanasansi mtupe majawabu" ameongeza Dkt. Jingu 


Dkt. Jingu pia ametoa rai kwa wadau kuendelea kuisaidia Serikali kutengeneza mazingira wezeshi yanayosaidia upatikanaji wa wanasayansi wenye uweledi na tija kwaajili ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu kama Maabara za kujifunzia.


Wakati wa hafla hiyo Dkt.Jingu ameipongeza Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kuona haja ya kuwapa motisha Wanafunzi ambao wamefanya Vizuri Zaidi Katika Masomo ya Sayansi. 


"Mkemia mkuu hili zoezi liendelee mara kwa mara, na liongezewe ubunifu ili kuzidi Kuibua hamasa kwa wanasansi chipukizi nafahamu Tangu 2007 tunatoa zawadi za kutambua mchango wa waliofanya vizuri katika masomo ya sayasi (Fizikia, Baiolojia na Kemia) na mwakani nmeambiwa tutaanza kutoa na hesabu" amesema Dkt. Jingu 


Kwa upande wake Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt. Fidelice Mafuniko amesema jumla ya wanafunzi 36 ambapo kwa kidato cha 4 ni vijana 18 na kidato cha sita ni vijana 18 wametunukiwa vyeti pamoja na walimu wao wa kidato cha Nne wa 4 na cha sita wawili huku Mwenyekiti wa Bodi


Kadio amesema liicha ya uwepo wa changamoto nyingi za kijamii, Afya na uchumi anamini sayansi na teknolojia ndio msingi mkubwa wa kukabilina na changamoto hizo


MWISHO