UNYONYESHAJI WATOTO NI NGUZO YA MAENDELEO YA TAIFA
Posted on: August 4th, 2025
Na. WAF, Dodoma
Wataalam wa fya na wadau wa mbalimbali wametakiawa kujadili sera na kutoa mapendekezo yenye tija ili kuweka mazingira wezeshi kwa mama kunyonyesha watoto bila kujali aina ya kazi wazozifanya ili kuweka nguzo imara afya kwa mtoto na maendeleo ya taifa kwa ujumla
Akizungumza leo Agosti 4, 2025 katika maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji yanayoadhimishwa kitaifa Jijini Dodoma, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Kinga Wizara ya Afya Dkt. Otilia Gowelle amesema wataalam wa afya wamejumuishwa kwenye maadhimisho hayo kwa lengo la kuwaongezea uelewa na kutoa hoja za kuongeza elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa mama kumnyonyesha mtoto.
Amesema maziwa ya mama yamebeba kinga na humuaandaa mtoto katika makuzi yenye afya yatakayoleta tija kubwa kwenye maendeleo ya kijamii na taifa kwa ujumla sababu ya kuwa na afya njema itakayorahisisha uwajibikaji kwenye nyanja nzima ya kifamilia bila hofu ya kuuguza mtoto.
“Hii ni sehemu ambayo sisi kama wataalam na wahudumu wa afya, tunapaswa kuona namna ambavyo hoja zetu zitasaidia kuoboresha na kuweka mazingira wezeshi kwa akina mama wanaonyonyesha iliyotuwezesha kuwa na jamii yenye afya bora, sababu mtoto akiumwa kila wakati hata kiwango cha utafutaji kinapungua kwenye familia,” amesema Dkt. Gowelle.
Aidha, Mkurugenzi wa huduma za lishe Wizara ya Afya Bi. Neema Joshua amewataka wanaume kutoa dhana potofu ya kuzuia wanawake kunyonyesha watoto kwa kigezo cha misuli ya matiti kusinyaa na kupoteza mvuto wao, akidai hiyo inapunguza jitihada za wadau na Serikali katika kuhakikisha watoto wanapata afya bora wanapozaliwa kwa kunyonya maziwa ya mama mpaka watakapotimiza miaka miwili.
Amesema, mabadiliko ya kimaumbile yapo na huja kutokana na umri wa mwanamke, hivyo hata asiponyonyesha mtoto kwa hofu ya matiti kupoteza mvuto wake, ikifika muda wa misuli kulegea matiti bado yatalala hata mtoto asipohusika kunyonya.
“Akina baba tushirikiane kwenye hili sababu hizi ni imani ambazo wengi wanaambizana huko mitaani, kuna vitu vingi vya kuvutia kwa mwanamke sio matiti yake pekee, hovyo kuzuia mtoto kunyonya ni kumdhulumu haki yake, " amesisitiza Bi. Joshua.