"TUUNGE MKONO KWA VITENDO JITIHADA ZA DKT. SAMIA KATIKA SEKTA YA AFYA ", DKT. MOLLEL
Posted on: November 20th, 2023Na. WAF, Dar es Salaam
Uwekezaji wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan
katika sekta ya afya utaongeza tija iwapo wahudumu wa sekta ya Afya nchini watatoa huduma bora zenye tija kwa wananchi.
Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Afya Dkt Godwin Mollel wakati akizungumza na watumishi wa hosptali ya rufaa ya mkoa ya Mwananyamala wakati wa ziara yake ya kikazi
Dkt. Mollel amewasisitiza watumishi wa kada ya afya nchini kuhakikisha wanaboresha huduma kwa kufuata misingi ya huduma kwa wateja ili wagonjwa wapatiwe huduma bora kuanzia waingiapo hospitalini
Dkt. Mollel amesema, baadhi ya wananchi hawafiki hosptali za serikali kutokana na kukosekana kwa huduma rafiki kwa wateja na kutaka pia walinzi wajengewe uwezo wa kujua namna bora ya kupokea wagonjwa badala ya kufokea ndugu za wagonjwa au wagonjwa wenyewe
"Tuna kazi moja ya kuhakikisha tunaboresha huduma kwa mteja, lugha zetu na kila kitu kikae vizuri", ameeleza Dkt. Mollel
Ametoa wito kuwa wajipange vizuri kwenye eneo la huduma kwa mteja ili kuleta tija ya uwekezaji uliofanywa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika sekta ya afya nchini .
Aidha Dkt.Mollel amesema kwa kipindi hiki Rais Dk.Samia Suluhu Hassan adaiwi chochote katika sekta ya afya, bali watoa huduma ndio wanadaiwa kutoa huduma bora kwa wananchi.
See translation