Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

TUJIKINGE DHIDI YA UGONJWA WA EBOLA” DKT MOLLEL

Posted on: October 7th, 2022

Naibu Waziri wa Afya, Mheshimiwa Dkt. Godwin Mollel amewataka wananchi kuchukua tahadhari juu ya mlipuko wa ugonjwa wa Ebola ambao umeripotiwa hivi karibuni katika Nchi jirani ya Uganda.

Dkt. Mollel amesema hayo alipokuwa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, Mkoani Geita katika ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya Afya inayotekelezwa katika ngazi ya Kata.

“Ni rahisi kuukwepa ugonjwa wa Ebola. Jufunzeni, fuateni taratibu mlizopewa kadri ya miongozo ya Afya iliyotolewa na Wizara ya Afya” amesema Dkt. Mollel.

Amewaasa wananchi kunawa mikono vizuri, kupunguza kusalimiana kwa mikono kwa sababu majimaji ya mwilini pamoja na damu ndio vyanzo vya kueneza ugonjwa wa Ebola.

Pamoja na hayo, Dkt. Mollel aliwahikikishia Wananchi wa Msalala kuwa Tanzania bado ipo salama lakini akasisitiza kuwa Tanzania itakuwa salama zaidi endapo kila mwananchi atafuata kanuni na miongozo ya Afya kadri ilivyotolewa na Wizara ya Afya.