Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

TANZANIA YANYAKUA TUZO YA GLOBAL IMPACT 2024

Posted on: June 9th, 2024



Na WAF- Marekani

Tanzania yapewa tunzo ya Global impact award 2024 kwa kazi kubwa zenye matokeo chanya zinazofanywa katika mapambano dhidi ya saratani ikiwemo chanjo ya HPV kwa wasichana, uchunguzi wa saratani ya matiti na mlango kizazi, usimikaji wa mashine za tiba mionzi, mashine za uchunguzi za CT scan, pamoja na PET CT Scan.


Tuzo hiyo imepokelewa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel June 8, 2024 imetolewa na Shirika la Global Health Catalyst la Marekani, akimuwakilisha Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa Mkutano na wadau wa sekta ya afya wanaojihusisha na mapambano dhidi ya ugonjwa wa Saratani

Akizunguza wa kati wa Mkutano huo Dkt. Mollel amesema Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuimarisha huduma za Afya nchini kwa kuboresha miundo mbinu, vifaa tiba vya kisasa na Wataalam wakutosha ikiwa ni jitihada za kupambana na ugonjwa wa Saratani.

Ameongeza kuwa Ushirikiano uliopo baina ya Serikali ya Tanzania na Marekani unasaidia kuboresha sekta ya afya na kusaidia watanzania kupatiwa matibabu ya ugonjwa wa Saratani hapa hapa nchini na kupunguza Rufaa za kwenda nchi za nje na kupelekea kupunguza gharama za matibabu kwa watanzania na kuongeza kuwa ushirikiano huo unalenga kukuza Tiba Utalii ndani ya nchi ya Tanzania.