TANZANIA KUFANYA UKAGUZI WA MELI KUDHIBITI MAGONJWA YA MLIPUKO
Posted on: October 22nd, 2025
Na WAF - DAR ES SALAAM
Wataalam 45 wa Afya kutoka mipaka ya bandari nchini wanashiriki mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kufanya ukaguzi wa meli kwa kutumia kanuni za Shirika la Afya Duniani (WHO) yenye lengo la kudhibiti magonjwa ya mlipuko kutoka nchi nyingine.
Mkuu wa Huduma za Afya Mipakani kutoka Wizara ya Afya Dkt. Amour Selemani akifungua mafunzo hayo leo Oktoba 21, 2025 Jijini Dar es Salaam amesema kanuni zitakazotumiwa na wataalam hao ni za mwaka 2005 (IHR 2005) zilizoidhinishwa na WHO na kuridhiwa na nchi wanachama wa shirika hilo ambapo meli zitakazotumia bandari za Tanzania na kukidhi vigezo zitapatiwa vyeti vya usafi wa mazingira.
Amesema mafunzo hayo yamehusisha wataalam kutoka Bandari za Dar es Salaam, Tanga, Mtwara, Mwanza, Kigoma na kwa upande wa Zanzibar ni Malindi, Wete, Mkoani,Fumba na Mkokotoni.
‘’Wizara ya Afya imeandaa mafunzo haya ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa hitaji la wataalam wenye uwezo wa kutambua nakudhibiti magonjwa ya mlipuko kama ilivyoagizwa na Naibu Waziri Mkuu Dkt. Doto Biteko wakati akifungua Mradi wa Uimarishaji Udhibiti wa Magonjwa ya Mlipuko Maarufu Pandemic Fund hivi karibuni Jijini Mwanza,” amesema Dkt.Amour.
Kuhusu vitendea kazi Dkt. Amour amesema tayari vifaa vinavyotumika kutambua na kudhibiti magonjwa kwa kuanzia vipo tayari na vingine vipo katika machakato wa kununuliwa kwa ufadhili wa WHO kupitia mradi wa Uhimarishaji Udhibiti wa Magonjwa ya Mlipuko unaotekelezwa na shirika hilo.
Naye Afisa Ufuatiliaji wa Magonjwa ya Mlipuko kutoka WHO-Tanzania Dkt. George Kauki amesema mafunzo kwa wataalam hao kimsingi yametumia hatua kadhaa ya kimaandalizi ikiwemo yale ya njia ya mtandao, yakifuatiwa na hatua ya pili ya wataalam kutoka Wizara ya Afya yaliyolenga kuwajengea uwezo kulingana na mazingira ya nchi.
Dkt. Kauki pia amebainisha kuwa ili wataalam hao wa Afya waweze kufanya ukaguzi na kutoa cheti inabidi wapate mafunzo kutoka kwa wataalam waliodhinishwa na WHO akieleza kuwa ni hatua muhimu inayoifanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza kwa ukanda wa maziwa makuu kuwa na wataalam wenye uwezo wa kufanya ukaguzi na kutoa vyeti kwa meli zitak