TANZANIA KUANZISHA PROGRAMU JUMUISHI YA KUWATUMIA WAHUDUMU WA AFYA NGAZI YA JAMII
Posted on: August 2nd, 2023TANZANIA KUANZISHA PROGRAMU JUMUISHI YA KUWATUMIA WAHUDUMU WA AFYA NGAZI YA JAMII
Tanzania inakusudia kuanzisha programu Jumuishi ya Kuwatumia Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii yenye lengo la kuharakisha upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wote hususan katika ngazi ya msingi.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu akiwa Geneva Uswisi akishiriki kikao kwa njia ya mtandao kilichoandaliwa na Shirika la Misaada na Maendeleo la Marekani (USAID) kwa kushirikiana na UNICEF kuhusu utekelezaji wa vipaumbele vya Azimio la Monrovia (2023) linalohusu Watoa Huduma wa Afya Ngazi ya Jamiii (Community Health Workers' Roadmap).
“Program hii inatarajia kuanza mwaka wa fedha 2023/24 na inalenga kuvifikia vijiji 12,318, mitaa 4,263 na vitongoji 64,384 nchi nzima” amesema Waziri Ummy.
Kikao hicho kimeshirikisha Mawaziri wa Afya, viongozi waandamizi wa Sekta ya Afya kutoka nchi 16 za Bara la Afrika na Asia na Mashirika ya Kimataifa kilijadili jinsi ya kuongeza rasilimali fedha, kuongeza ufanisi na tija katika utekelezaji wa miradi ya kuwatumia Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii.