Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

SERIKALI, WADAU TUIMARISHE HUDUMA ZA AFYA YA MACHO.

Posted on: September 11th, 2024

Na WAF- Dodoma 


Serikali imesema inaweka mikakati  ambavyo itaweza kuiendeleza na kuhakikisha kuna takwimu na taarifa sahihi juu ya huduma za afya ya macho nchini  sambamba na kutilia mkazo mfuko wa bima ya Afya kwa wote 


Hayo yamesemwa na Dkt Caroline Damian Kaimu Mkurugenzi wa Tiba Wizara ya Afya leo septemba 11, 2024 katika ufunguzi wa kikao kazi Kati ya waratibu wa afya ya macho mikoa pamoja na wadau wa macho kilichofanyika mkoani Dodoma.


“Kama tutapata kila kitu miundombinu, vifaaa pamoja na vifaa tiba lakini tukashindwa kusimamia  ubora tutakuwa hatuna kazi tunayoifanya hivyo inatubidi kusimamia ubora wa huduma za afya ya macho.” Amesema Dkt Caroline 



Kwa upande wake Dkt. Paul Chaote Mkurugenzi msaidizi wa maswala ya afya Ofisi ya Rais Tamisemi amesema inatakiwa kuwa na usawa kwa wadau wakati wa  utoaji wa hiduma kwenye  maeneo tunayofikisha huduma ili


“Katika eneo  la macho na meno ni maeneo ambayo yanaendelea  kufanya vizuri lakini  kumekuwa na changamoto ya watumishi bobezi tukija katika ajira hakuna wataalam hivyo niwaombe ndugu zetu wadau kwa sekta hii ya afya ya macho mliangalie hili ili tuweze kuongeza idadi kubwa ya wataalamu na a” Amesema Dkt.. Chaote


Sisi Kama serikali kupitia ofisi ya Rais TAMISEMI tutaendelea kushirikiana ili tuweze kufikia wananchi kwa urahisi na kuboresha upatikanaji wa huduma hizi za afya ya macho kwani maeneo yote yalio na mahitaji makubwa.


Akizungumza katika mkutano huo Bw.  Edson Mwampopo mdau kutokea taasisi ya KCCO  amesema wadau wanapata ushirikiano mzuri kutokea Wizara ya Afya katika kutekeleza miradi ambayo wanaisimamia 


Mwakilishi wa Waratibu wa Afya ya macho ngazi ya mkoa kutoka  Pwani Dkt Mzava amesema anawaomba wadau kuendelea kushirikiana katika sekta ya afya na wizara ya afya ili kuhakikisha urahisi wa uratibu wa sekta hiyo ya afya. 


“Kuna baadhi ya mikoa ambayo haina wadau na mingine ina wadau wachache hivyo tunasisitiza ushirikiano wenu ili kurahisisha na kuimarisha huduma hizo za afya ya macho kwa wananchi.”Amesema Dkt Mzava