Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

SERIKALI ITAENDELEA KUSIMAMIA UTEKELEZAJI WA SERA YA AFYA INAYOTOA MSAMAHA WA MATIBABU

Posted on: May 14th, 2024



Na WAF - Dodoma

Serikali kupitia Wizara ya Afya itaendelea kusimamia Sera ya Afya ya mwaka 2007 inayotoa msamaha wa huduma za matibabu kwa makundi mbalimbali ikiwemo kina mama wajawazito.

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema hayo leo Mei 14, 2024 wakati akijibu swali namba 333 la Mbunge wa Vitu Maalum Mhe. Esther Edwin Malleko alipouliza “Je, lini huduma ya Ultrasound itatolewa bure kwa wajawazito wanapohudhuria kliniki.”

Waziri Unmy amesema, katika kuondoa vikwazo vya upatikanaji wa huduma za Afya kwa wananchl, Serikali imepitisha Sheria ya Bima ya Afya kwa wote ambayo itawawezesha makundi yote kupata huduma za vipimo na matibabu
bila kikwazo cha fedha.

Aidha, Waziri Ummy amesema Serikali inatarajia kutumia shilingi Bilioni Mia 500 ili kuboresha miundombinu katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili ikiwa ni muendelezo wa Serikali kufanya hospitali hiyo kupanua matibabu ya kibingwa.

Amesema, kwa sasa Serikali inaendelea na hatua za kuiboresha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ili kuweza kutoa huduma zote za matibabu ya kibingwa na ubingwa bobezi bila kutegemea Hospitali nyingine.

Waziri Ummy Ummy amesema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Konde Mhe. Mohamed Said Issa aliyeuliza “Je, lini Serikali itakuwa na Hospitali kuu ya Taifa moja ambayo itakuwa ikitoa huduma zote za Afya bila ya kutegemea Hospitali nyingine.

“Tayari Serikali ina Hospitali ya Taifa ambayo ni Hospitali ya Taifa Muhimbili ambayo kwa sasa hatua za kuiboresha Hospitali hiyo zinatekelezwa ili kuweza kutoa huduma zote za matibabu ya kibingwa na ubingwa bobezi ambayo itakua ni Hospitali moja ya Taifa itakayo kuwa inatoa huduma zote za Afya bila kutegemea Hospitali nyingine.” Amesema Waziri Ummy