Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI CHANJO MOJA INAJITOSHELEZA

Posted on: April 13th, 2024


Na WAF – Dodoma.

Tafiti zilizofanywa dhidi ya chanjo ya saratani ya shingo ya mlango wa kizazi nchini zinaonyesha dozi moja ya chanjo inaweza kutoa kinga ya kutosheleza sawa na dozi mbili.

Hayo yamesema Mkurugenzi wa idara ya huduma za afya ya uzazi mama na mtoto Wizara ya Afya Dkt. Ahmed Makuwani leo Aprili 13, 2024 wakati wa ufunguzi wa kikao cha tathmini na maandalizi ya utoaji wa chanjo ya Saratani ya mlango wa kizazi jijini Dodoma. 

Dkt. Makuwani amesema mabadiliko haya yataongeza ufanisi na kuongeza kuchanja wasichana wengi zaidi hivyo kutosheleza kundi kubwa la mabiti wenye umri kuanzia miaka tisa hadi kumi nanne na yatapunguza uasi wa chanjo hiyo kuinua hali ya uchanjani wa chanjo ya HPV.

“Wakati tunatoa dozi mbili za chanjo ya HPV, Lengo la chanjo ya kwanza ilikuwa inafikia asilimia 85 sasa hivi kwa kuwa tunakwenda kuweka umakini kwenye utoaji wa dozi mmoja itawezesha kuwafika walengwa ambao ni mabinti wenye umri wa miaka tisa hadi kumi na nne kwa wingi zaidi”. Amesema.

Ameeleza kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoongoza kuwa na kiwango kikubwa cha Saratani ya mlango wa kizazi ulimwenguni na ndio saratani inayoongoza kusababisha ugonjwa na vifo vya akinamama nchi.

Dkt. Mkuwani amewataka walimu kote nchini kusaidia kuhamasisha na kutoa elimu kwa jamii ili kurahisisha utoaji wa huduma hii na kuongeza ufanishi wa utoaji wa chanjo hii.

“Ninawapongeza walimu kwa kujitokeza najua mtaibeba ajenda hii na kwenda kuhamasisha wazazi pamoja na walengwa ambao ni mabinti kujitokeza kupatiwa chanjo hii kwa sababu walimu ndio mnaokaa na mabinti kaa muda mrefu.

Dkt. Makuwani amewashukuru wadau wa maendeleo wa sekta ya Afya nchi kwa mchango wao katika kuhakikisha mabinti wa kitanzania wanapatiwa chanjo hii ya saratani ya mlango wa kizazi.

Mwisho.