Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

RAIS SAMIA KINARA WA AJENDA ZA KUINUA WANAWAKE - DKT. MPANGO

Posted on: April 6th, 2024


Na WAF - Dar Es Salaam


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango amesema, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, amekuwa mstari wa mbele kusukuma ajenda za kumkomboa mtoto wa kike kwenye changamoto zinazo mkabili.


Dkt. Mpango, ameyasema hayo alipokuwa akifungua mkutano wa masuala ya uongozi kwa wanawake kisekta Aprili, 06, 2024 jjiini Dar es salaam kwenye ukumbi wa kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere.


Amesema, uwekezaji mkubwa umefanywa kwenye Sekta ya Afya, Maji, Elimu na Nishati zimekuwa jitihada za makusudi za kumuinua mtoto wa kike kutokana na baadhi ya changamoto zilizokuwa zinawakabili kwa kipindi kirefu ikiwepo mila potofu pamoja na mfumo dume uliokuwa umeshamiri miongoni mwa baadhi ya jamii.


“Jitihada hizo upande wa Sekta ya Afya, kupitia huduma inayotekelezwa na mpango wa M-mama umewezesha kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi, kutoka vifo 556 kwa kila vizazi hai 100,000 mwaka 2016 hadi kufikia vifo 104 kwa kila vizazi hai 100,000 kwa sasa.” Amesema Dkt. Mpango 


Kuhusu sekta ya maji, “Mhe. Rais amefanya jitihada za kumtua mama ndoo kichwani kwa kuhakikisha huduma ya maji inapatikana kwa uhakika na kumpunguzia adha mama kufuata maji umbali mrefu, kwani ameongeza bajeti ya maji kutoka shilingi bilioni 709.4 kwa mwaka wafedha 2022/23 hadi kufikia shilingi bilioni 756.2 kwa mwaka fedha 2023/24”. Amesema Dkt. Mpango.


Dkt. Mpango amesema, Serikali imedhamiria kuwa na nishati safi na salama kwa mazingira salama kwa jamii, ambapo shabaha ya serikali nikuhakikisha ifikapo 2030 matumizi ya nishati iliyo safi na salama kwa mazingira inafikia asilimia 80 na hususan ni maeneo ya vijijini ambapo matumizi ya nishati isiyo rafiki imekithiri.


Kuhusu elimu Makamu wa Rais Dkt. Mpango, amesema zimekuwepo jitihada zenye tija kwa watoto wa kike kwa kuwajengea Shule Maalumu za Bweni ili waweze kuhitimu masomo yao na kufikia matamanio yao ya kile wanachotaka kufanya katika maisha yao.


“Wapo baadhi ya watoto wa kike walikuwa wamepata ujauzito na kujifungua watoto, Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan imehakikisha, wanarudi shuleni hata baada yakujifungua na kuendelea na masomo” Amesema Dkt. Mpango,


Akimkaribisha Makamu wa Rais kufungua mkutano huo, Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu, amesema mkutano huo imekuwa ni heshima kwa nchi kupokea, kwani ni kwa mara ya pili unafanyika katika bara la Afrika awali ulifanyika nchini Rwanda. 


“Kutokana na Nchi kufanya vizuri katika vile viashira vikuu vyakupima afya Duniani kwani kama nchi tumeweza kupunguza vifo vya mama wajawazito kwa Zaidi ya asilimia 80 kwani mbali yakupunguza vifo vya zizazi hai lakini pia kwa upande wa vifo vya watoto wa chini ya miaka mitano kutoka vifo 67 hadi vifa 45 kati vizazi 1000” Amesema Mhe. Ummy.


Nae, Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. John Jingu amesema, suala la Afya hakuna wakuachwa nyuma kwa wanawake na wanaume Ili tuweze kufanikiwa kwenye Afya”. Amesema Dkt. Jingu