PROF. NAGU ATAKA MAONI YATAKAYO ISADIA SEKTA YA AFYA JUMUIYA AFRIKA MASHARIKI
Posted on: April 30th, 2024
Na WAF, Dar Es Salaam.
Mganga Mkuu wa Serikali wa Prof. Tumaini Nagu, ametoa rai kwa wataalamu wa sekta ya Afya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kutoa maoni yatakayosaidia Jumuiya kuimarisha miundombinu ya huduma ya afya na kukabiliana na matishio ya kiafya kwa magonjwa yanayoambukiza na yasiyoambukiza.
Prof. Nagu ametoa kauli hiyo Aprili 30,2024 Jijini Dar Es Salaam katika ufunguzi wa Mkutano wa Kawaida wa 24 wa Baraza la Mawaziri wa sekta ya Afya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) .
“Tumekuja kujadili na kutoa suluhisho na majawabu yatakayo wezesha kukabili changamoto za kiafya ndani ya nchi za Jumuiya yetu kwa kuzingatia ubunifu na weledi wa mifumo yetu ya afya huku tukiwa na umoja wenye nguvu zaidi” amesema Prof. Nagu
Prof. Nagu amehimiza umuhimu wa Sekta ya Afya kwa Jumuiya kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi na umoja wakati wa utekelezaji progamu mbalimbali za Afya ikiwemo miradi ya Sekta ya Afya na mikakati inayopangwa ili kufikia mafanikio yanayotarajiwa kwa wakati.
Mbali na kufanya tathimini ya utekelezaji wa maagizo na makubaliano yaliyofikiwa katika mkutano wa 22 wa Baraza hilo, Mkutano huo utajadili agenda nyingine ikiwemo Mkutano na taarifa za Vikundi Kazi (Technical Working Group – TWG) sita (06) vya Sekta ya Afya na mapendekezo ya Tanzania kuanzisha Kituo cha Umahiri cha Upandikizaji Uloto na Sayansi ya Matibabu ya Magonjwa ya Damu chini ya Hospitali ya Benjamin Mkapa.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Sekta ya Jamii wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dkt. Irene Isaka, ameeleza kuwa kupitia mkutano huo nchi wanachama watapata fursa ya kusikia taarifa zitakazowasilishwa na kila nchi ili kwa pamoja kuweza kuchangia na kushauri namna bora ya kusimamia na kutekeleza programu, miradi na miundombinu ya Afya katika Jumuiya.
Mkutano huo wa siku tano, unafanyika kwa njia ya mseto (video na ana kwa ana) umeanza kwenye ngazi ya wataalam ukilenga kufanya tathimini ya utekelezaji wa maagizo na makubaliano yaliyofikiwa katika mkutano wa 22 wa Baraza hilo.
Mkutano utafuatiwa na ngazi ya Makatibu Wakuu tarehe 2 Aprili 2024, ambapo taarifa itawasilishwa, Makatib