NAIBU MWAKILISHI WA UNICEF NCHINI AAGA WIZARA YA AFYA
Posted on: May 31st, 2024
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. John Jingu mapema leo tarehe 31 Mei 2024 amepokea ugeni wa aliyekua Naibu Mwakilishi wa Shirika la UNICEF nchini Tanzania Bw. Ousmane Niang ambaye amefika ofisini hapo kwa lengo la kuaga baada ya kuhamishiwa nchini Benin kama Mwakilishi Mkazi wa UNICEF nchini humo.
Katika Mazungumzo yao Katibu Mkuu Dkt. John Jingu, amemshukuru Kiongozi huyo kwa muda wote ambao alifanya kazi nchini na kuahidi kuendelea kudumisha ushirikiano huo katika kuwahudumia Watanzania hususan ni kwenye sekta ya Afya.
Naye Bw. Niang ameishukuru Wizara ya Afya kwa ushirikiano mzuri na UNICEF hususan katika eneo la kukabiliana na dharura na majanga ya kijamii ambapo katika kipindi alichohudumia nchini ameweza kushirikiana kikamilifu katika kukabiliana na majanga kama mlipuko wa ugonjwa wa Maburg Mkoani Kagera na Mafuriko ya Katesh Mkoani Manyara.
Tukio hilo limefanyika katika Ofisi za Wizara jijini Dodoma na kuhudhuriwa pia na Wakurugenzi na Maafisa wa Wizara ya Afya