Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

MPANGO JUMUISHI WA WAHUDUMU WA AFYA NGAZI YA JAMII WAENDELEA KWA MANUFAA MAKUBWA

Posted on: September 25th, 2025

Na WAF, Ruvuma

Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bi. Hilda Ndambalilo amesema kuanza kaI kwa Wahudumu wa Afya wa Ngazi ya Jamii imekuwa ni manufaa kwa jamii kwani elimu kuhusu Kujilinda na magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza, lishe, usafi wa mazingira, afya ya mama na mtoto, utoaji wa rufaa pamoja na upimaji wa magonjwa kama kisukari, shinikizo la damu na uzito vimekuwa na tija kubwa.

Bi. Ndambalilo amesema hayo leo Septemba 23, 2025 baada ya kupokea timu ya wataalam kutoka Wizara ya Afya na Ofisi ya Rais-TAMISEMI iliyofika kufanya usimamizi shirikishi wa utekelezaji wa mpango jumuishi wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii ili kuimarisha utekelezaji wa zoezi hilo.

"Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii wamekuwa mkombozi mkubwa kwenye eneo la afya ngazi ya jamii kwani kutokana na kutoa elimu, kuhamisisha jamii kuhusu mambo mbalimbali ya afya imeleta mageuzi anuwai" amesema Bi. Ndambalilo.

Naye Mratibu wa Huduma za Afya Ngazi ya Jamii kutoka Wizara ya Afya Dkt. Norman Jonas amesema Serikali inaendelea kuimarisha huduma za afya ngazi ya jamii kwa kuhakikisha Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii wanapatiwa vitendea kazi ikiwemo mashine za kupima sukari na presha, vishikwambi (Tablet), sare na kuhakikisha wanapata malipo yao kwa wakati ili kurahisisha utendaji kazi wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii.

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Ofisi ya Rais - TAMISEMI kwa kushirikiana na Wadau wanaendelea kutekeleza afua za kuimarisha utoaji wa huduma za afya Ngazi ya Jamii kupitia Mpango Jumuishi wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii (CHW) ambao ulizinduliwa na Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, MPANGO JUMUISHI WA WAHUDUMU WA AFYA NGAZI YA JAMII WAENDELEA KWA MANUFAA MAKUBWA

Na WAF, Ruvuma

Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bi. Hilda Ndambalilo amesema mara baada ya Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii kuanza kazi kumekuwa na manufaa kwa jamii kwani elimu kuhusu kujilinda na magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza, lishe, usafi wa mazingira, afya ya mama na mtoto, utoaji wa rufaa pamoja na upimaji wa magonjwa kama kisukari, shinikizo la damu na uzito vimekuwa na tija kubwa.