Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

MADAKTARI BINGWA, HUDUMA ZA KIBINGWA ZAMU YA TABORA KWA HALMASHAURI ZOTE NANE

Posted on: June 10th, 2024Na WAF, TABORA

Madaktari Bingwa wa Rais Samia wapatao 40 wamepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Paul Chacha shabaha ikiwa ni kutoa huduma za kibingwa kwa wananchi kupitia kambi ya siku tano katika hospitali za wilaya za halmashauri nane za mkoa wa Tabora.

Akizungumza nao Juni 10, 2024 wakati wa hafla yakuwapokea na kuwaaga kwenda katika Hospitali za wilaya, Mkuu wa Mkoa Chacha amesema hiyo ni fursa adhimu kwa mkoa wao, hivyo watahimizana ili siku tano za huduma zilizo pangwa ziwe na matokeo chanya kwa mkoa huo na kuahidi ushirikiano wa moja kwa moja kwa Madaktari bingwa hao kipindi chote watakachokuwa katika mkoa huo.

"Tabora kwetu hii ni fursa adhimu, tunatambua kabisa kwa huduma hizi mlizo zileta zinaakisi mapenzi mema ya Rais wetu Dkt. Samia katika sekta ya Afya hususani kuwajali wananchi wa kipato cha chini" amesema Chacha.

Chacha ameongeza kuwa, huduma hizo kama sio maono ya Dkt. Samia yakuwafikia wananchi, ingelazimu kuzifuata Mwanza, Dar es Salaam au wakati mwingine KCMC, hivyo ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa ajili ya kuangalia afya zao na kupata matibabu pale itakapo lazimu.

Naye Katibu Tawala mkoa wa Tabora Dkt. John Mboya, amesema mkoa huo ndani ya kipindi cha miaka mitatu huduma za Afya zimeimarika upande wa miundombinu na vitendea kazi sambamba na wataalam wa Afya mara baada yakupokea kiasi cha shilingi bilioni 29.3 ndani kipindi cha miaka mitatu

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa mkoa Bi. Honoratha Rutatinisibwa akitoa taarifa ya madaktari walio wapokea amesema watakuwepo katika mkoa huo kwa muda wa siku tano kuanzia Juni 10 hadi 14,2024

"Mhe.Mkuu wa Mkoa kati ya Madaktari Bingwa 40, tuliowapokea kila wilaya itapata nadaktari watano wakiwepo wa Usingizi, Magonjwa ya wanawake,Magonjwa ya watoto Magonjwa ya ndani pamoja na upasuaji