Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

MADAKTARI BINGWA 45 WA DKT SAMIA KUWEKA KAMBI SIKU TANO KATIKA HOSPITALI ZA HALMASHAURI TISA MKOANI PWANI

Posted on: June 3rd, 2024



Na WAF - Pwani

Mkuu wa mkoa wa Pwani, Mheshimiwa Abubakar Kunambi, mspema leo tarehe 03 Juni,2024 amewapokea madaktari bingwa arobaini na tano (45) ambao watakwenda kutoa huduma za kibingwa katika hospitali za halmashauri za wilaya tisa za mkoa Pwani, madaktari Bingwa wa Samia watatoa huduma kwenye Hospitali za Halmashauri tisa mkoani Pwani kuanzia leo tarehe 3 Juni, 2024 hadi 07 Juni, 2024.

Mkuu wa mkoa Kunambi wakati wa kuwapokea Madaktari Bingwa maarufu kama Madaktari Bingwa wa Dkt. Samia kwenye ukumbi wa mikutano Ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Pwani amesema "Madaktari hawa wataongeza nguvu katika kuboresha huduma za afya na kuongeza upatikanaji wa huduma za kibingwa kwa wananchi wa maeneo ambayo kulikuwa hakuna Madaktari Bingwa, Pia hii ni hatua muhimu katika kuhakikisha huduma bora za afya zinawafikia wananchi wengi zaidi kwa urahisi na ufanisi"

Aidha, ameongeza kwa kusema kuwa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya Afya na Kazi kubwa na mafanikio makubwa ya uwekezaji katika kuboresha miundo mbinu na vifaa tiba imefanyika katika Hospitali za wilaya hivyo ujio wa Madaktari Bingwa wa Samia unakuja kuchagiza zaidi kuboresha Huduma moja kwa moja kwa wanaanchi waliopo katika maeneo ambayo hakuna hao madaktari Bingwa, hivyo wanaanchi wanapaswa kuchangamkia hii fursa ambayo mhe.Rais Samia amewasogezea Huduma za kibingwa ambazo wangelazimika kufuata umbali mrefu.

Pia Mratibu kutoka Wizara ya Afya ndugu Meena amesema " Serikali ya awamu ya Sita chini ya Mhe. Dkt Samia kupitia wizara ya afya wamedhamiria kuhakikisha huduma za kibingwa zinawafiki wananchi wote kwa usawa 6kupitia mpango huu wa Madaktari Bingwa wa Samia ambao unaratibiwa kila mkoa na kila wilaya za mikoa yote Tanzania Bara.