Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

KIWANDA CHA DAWA CHA TPI KUANZA UZALISHAJI DAWA ZA ARV NCHINI IFIKAPO JUNI, 2026

Posted on: January 27th, 2026

Na WAF, Arusha

Waziri wa Afya Mhe. Mohamed Mchengerwa ameagiza uongozi wa kiwanda cha dawa cha Tanzania Pharmaceutical Industries Limited (TPI) kilichoko Njiro jijini Arusha kuanza kuzalisha dawa za kufubaza virusi vya UKIMWI (ARVVs) ifikapo mwezi Juni 2026 ili kupunguza mzigo wa kuagiza dawa nje ya nchi.

Waziri Mchengerwa amesema hayo Januari 27, 2025 wakati alipofanya ziara ya kutembelea kiwanda hicho ambacho kilisitisha uzalishaji tangu mwaka 2013.

Waziri Mchengerwa amesema kiwanda hicho chenye uwezo wa kuzalisha dawa 1,700,000 ndani ya saa 10 kilisamama kuzalisha kutokana na kukwamishwa na baadhi ya watu ambao hawakua na nia njema kwa nchi na kujali maslahi yao binafsi.

Waziri Mchengerwa amesema hivi sasa nchi inategemea kuagiza dawa nje ya nchi kwa asilimia 90, hapi inayolwamisha mipango mingi ya maendeleo.

Waziri Mchengerwa ameonya kwa mtu au taasisi yeyote itakayothubutu kukwamisha mchakato kuwa hata ivumilia na badala yake itahesabika kama mpinga maendeleo.

"Ninamuagiza Katibu Mkuu, kutenga Bilioni 20 kwa ajili yakuanza shughuli za uzalishaji wa dawa ifikapo mwezi Juni, lakini asitokee mtu akaturudisha nyuma huyo Sinto mvumilia", amesema Waziri Mchengerwa.

Kiwanda cha dawa cha Tanzania Pharmaceutical Industries Limited (TPI) kilianzishwa mwanzoni mwa miaka ya themanini na kufanyiwa maboresho makubwa 2013 hata hivyo kimekuwa katika mkwamo wa uzalisha tangu mwaka huo hadi hivi leo tamko la Serikali likivyotolewa..