JOGGING CLUB', ZINA MCHANGO MKUBWA MAPAMBANO DHIDI YA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA
Posted on: December 2nd, 2024Na WAF, DSM
Mkurugenzi msaidizi wa Magonjwa yasiyoambukizwa Dkt. Omary Ubuguyu amepongeza wadau wa mazoezi na vikundi vya Jogging kwa namna wanavyo hamasisha mapambano dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza kwa hamasa ya mazoezi.
Dkt Ubuguyu ametoa pongezi hizo Novemba 30, 2024 wakati wa Maadhimisho ya Miaka 10 ya Shirikisho la vyama vya Magonjwa Yasiyoambukiza nchini ambayo yamefanyika Coco Beach, jijini Dar es Salaam.
Dkt. Ubuguyu amewapongeza na kuwashukuru vijana, vikundi vya jogging club ikiwepo ile ya Wassafi na kwa namna ambavyo wanahamasisha mapambano dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza pamoja na kuleta hamasa ya mazoezi.
Dkt. Ubuguyi ameishukuru Taasisi ya Tanzania Non Communicable Diseases Alliance (TANCDA) kwa ushirikiano Mkubwa wanaoutoa kwa Serikali katika Mapambano dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza.
Pamoja na Juhudi hizi za kupambana na magonjwa yasiyoambukiza washiriki wamehimizwa kushiriki katika kuhamasisha watanzania wengi kujiunga na Bima ya Afya ili kupunguza mzigo wa gharama za matibabu ya magonjwa hayo.
Maadhimisho hayo yalitanguliwa na mchakamchaka (jogging) kutoka viwanja vya Coco beach kupitia Daraja la Tanzanite na kurejea Coco Beach na kuhusisha vikundi zaidi ya 10 pamoja na washiriki wengine kutoka taasisi za Serikali na kiraia pamoja na wanafunzi kutoka shule za Zanaki, Arabia na Shaaban Robert zote za jijini Dar es Salaam.