Customer Feedback Centre

Ministry of Health

JENGENI UTAMADUNI WAKUCHANGIA DAMU - MHE. SENDIGA

Posted on: June 14th, 2024



Na WAF - Manyara


Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Queen Sendinga, ametoa wito kwa wananchi wa mkoa huo na watanzania kwa ujumla kujenga mazoea ya kuchangia damu ili kuwasaidia watu wenye uhitaji wa damu.


Mhe. Sendinga ameyasema hayo leo Juni 14, 2024 Mkoani Manyara wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya wachangia damu Duniani, enye kauli mbiu ni isemayo “Kusherekea Miaka 20 ya Uchangiaji, Asanteni Wachangia Damu.” Ambapo Mhe. Sendinga amewasihi wananchi, Viongozi wa mitaa na vijiji, viongozi wa dini na taasisi mbalimbali kuwa mstari wa mbele kujitokeza kuchangia damu kwa hiari kwa ajili ya kuokoa maisha ya wagonjwa wenye uhitaji.


“Ili kuhakikisha kwamba kila mgonjwa anayehitaji tiba ya damu anapata damu salama, Shirika la Afya Duniani linapendekeza kukusanya chupa za damu asilimia 1 ya idadi ya wananchi waliopo kwenye eneo husika.” amesema Mhe. Senginda.


“Wengi wetu tunajua kuwa wachangia damu huokoa maisha kila siku kupitia zawadi yao ya uhai kupitia uchangiaji wa damu. Kila sekunde duniani, kuna mgonjwa anayesubiri kuwekewa damu ili aendelee kuishi, kama mnavyofahamu hapawezi kuwa na zawadi kubwa maishani kuliko zawadi ya uhai ” amesema Mhe. Senginda.


Amesema Lengo la serikali ni kuhakikisha kuwa kunakuwa na kituo cha damu salama kila mkoa na kila halmashauri inakuwa na timu ya ukusanyaji damukwa kuendelea kuimarisha timu na kuhakikisha hakuna mgonjwa anakosa damu pindi anapohitaji


“Maadhimisho ya mwaka huu yatatumika kufanya uzinduzi wa utengenezaji wa mazao ya damu katika vituo vya mikoa ya Manyara na Kigoma. Hii ni katika jitihada za kuongeza uzalishaji wa mazao ya damu ili iweze kusaidia katika utoaji wa huduma za kibingwa na bobezi ikiwa ni pamoja na upandikizaji wa viungo,” amesema Mhe. Sendinga.


Kwa upande wake, Meneja Mpango wa Taifa wa Damu Salama, Dkt. Abdul Juma Bhombo, amesema pamoja na jitihada zinazofanyika katika mkoa za kupunguza vifo vya akina mama wajawazito wakati wa kujifungua vinavyosababishwa na kupoteza damu nyingi, bado kuna vifo vya akina mama ambapo kwa mwaka 2023 kulikuwa na vifo 34 sawa na vifo 69 kati ya vizazi hai 1,000.