Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

ILI TUWAPUNGUZIE KAZI VIONGOZI WAJAO NI LAZIMA TUWEKEZE KWENYE LISHE BORA.

Posted on: August 29th, 2023

Na WAF- Dom.


Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel ametoa wito kwa Wataalamu wa afya kulipa uzito unaostahili suala la lishe ili wananchi waone umuhimu wake katika kuchangia mapambano dhidi ya magonjwa na kuleta tija katika maendeleo kwa mtu binafsi na kwa taifa kwa ujumla.


Dkt. Mollel amesema hayo leo Agosti 29, katika Mkutano wa tathimini ya saba ya utekelezaji wa Mkataba wa lishe ulioongozwa na Waziri wa OR TAMISEMI Mhe. Angellah Kairuki na kuhudhuriwa na Wakuu wa Mikoa, Makatibu tawala, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Waganga Wakuu wa Mikoa pamoja na Maafisa lishe nchini. 


"Ili tuwapunguzie viongozi wajao kazi ni lazima tuwekeze nguvu ya kutosha kwenye eneo la lishe." Amesema Dkt. Mollel. 


Ameendelea kusisitiza lishe sio suala la wajawazito pekee yake na watoto, bali hata makundi mengine ni muhimu kupata lishe bora itayosaidia kutunza afya na kuongeza miaka mingi zaidi ya kuishi.