HUDUMA ZA KIBINGWA NA BOBEZI ZIMELETA MATOKEO CHANYA HOSPITALI YA TEMEKE
Posted on: August 24th, 2023
Huduma za kibingwa na bobezi zimeleta matokeo chanya kwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke, kwa kufanya upasuaji wa kutoa saratani ya figo bila kuondoa figo nzima.
Upasuaji huo umefanyika leo katika Hospitali hiyo chini ya Madaktari Bingwa wa upasuaji wa jumla na mfumo wa mkojo, Dkt. Hussein Msuma na Daktari Msaidizi Dkt. Hamis Mbarouk
Upasuaji huo umeenda vizuri bila changamoto yoyote na wiki moja iliopita hospitali hiyo ilifanikiwa kufanya upasuaji wa kutoa jiwe kwenye Figo ambao pia ni upasuaji wa kwanza kufanyika hospitalini hapo.
Kufanyika kwa Huduma za upasuaji mkubwa huo ni matokeo chanya ya uwekezaji wa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassani alofanya katika hospitali hiyo hususani usimikaji wa vifaa tiba vya kufanyia upasuaji wa Huduma za kibingwa na kibingwa bobezi
Aidha, hospitali inaendelea kuboresha utoaji wa huduma kwa kuhakikisha huduma zote za kibingwa na kibingwa bobezi zinapatikana katika Hospitali hiyo bila kutoa rufaa.