HUDUMA ZA BENJAMIN MKAPA ZAMKOSHA SPIKA WA COMORO
Posted on: September 3rd, 2024Na WAF, Dodoma
Spika wa Bunge la Visiwa vya Comoro, Mhe. Moustadroine Abdou, amefurahishwa na huduma zinazotolewa katika Hospitali ya Kanda ya Benjamin Mkapa, kwa kuwa na huduma bora na uwekezaji mkubwa uliofanywa na serikali katika kuisaidia jamii kuendelea kuwa na afya bora.
Mhe. Abdou amefanya ziara hiyo leo Septemba 03, 2024 na kuongozwa na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, kwa lengo la kuangalia huduma zinazopatikana katika hospitalihiyo katika maeneo ya MRI, kitengo cha upandikizaji wa uroto, Kitengo cha upasuaji wa Moyo na Kliniki na wodi za watu maalumu.
Katika ziara hiyo, Mhe. Abdou ameridhishwa na kiwango cha huduma kinachotolewa na hospitali hiyo…
[15:14, 03/09/2024] Domina Field MoH: SPIKA WA COMORO, MHE. MOUSTADROINE ABDOU, AFURAHIA HUDUMA ZA HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA
Na WAF, Dodoma
Spika wa Bunge la Visiwa vya Comoro, Mhe. Moustadroine Abdou, amefurahishwa na huduma zinazotolewa katika Hospitali ya Kanda ya Benjamin Mkapa, kwa kuwa na huduma bora na uwekezaji mkubwa uliofanywa na serikali katika kuisaidia jamii kuendelea kuwa na afya bora.
Mhe. Abdou amefanya ziara hiyo leo Septemba 03, 2024 na kuongozwa na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, kwa lengo la kuangalia huduma zinazopatikana katika hospitali hiyo katika maeneo ya MRI, kitengo cha upandikizaji wa uroto, Kitengo cha upasuaji wa Moyo na Kliniki na wodi za watu maalumu.
Katika ziara hiyo, Mhe. Abdou ameridhishwa na kiwango cha huduma kinachotolewa na hospitali hiyo, akiishukuru
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uwekezaji mkubwa uliofanywa katika kuboresha sekta ya afya nchini na kusisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano kati ya Visiwa vya Comoro na Tanzania, hasa katika sekta ya afya pamoja na nyanja nyingine muhimu.
“Nina furaha kubwa kuona kiwango cha huduma kinachotolewa hapa. Tunathamini juhudi za Serikali ya Tanzania katika kuboresha sekta ya afya. Tunatumai kwamba ushirikiano huu utaendelea kuimarishwa, na utafaidisha wananchi wetu kwa pande zote”. Amesema Mhe. Abdou
Kwa upande wake, Naibu waziri wa afya Dkt. Godwin Mollel amemshukuru spika wa Bunge la Comoro kwa kufanya ziara katika hospitali hiyo ya BMH na kujionea huduma bobezi ambazo zinapatikana pia hata katika mataifa ya Ulaya na India na kusema kuwa kwa Nchi za Africa hakuna tena sababu kubwa za kwenda huko na hivyo kufika Tanzania na kupata huduma hizo bobezi na Teknolojia za kisasa wataalamu wetu walizonazo
“karibu sana katika hopitali zetu nyingine za taifa hospitali yetu ya Taifa Muhimbili na pia Mloganzila hapa tulipo ni hopitali ya kanda na sasa tunataka tuipeleke iwe hospitali ya Taifa katika hospitali zetu za Taifa kuna huduma bobezi za kutosha ulizoziona hapa na chache ambazo haukuziona hapa.”Amesema Dkt. Mollel
Pia Dkt. Mollel amesema serikali ipo tayari kuendelea kushirikiana na Serikali ya Comoro kwani wamekuwa wakishirikiana katika upande wa matibabu ya wagonjwa lakini pia wataendelea kushirikiana kwa kupeleka madaktari Comoro na madaktari wa Comoro kuja Tanzania kwa ajili ya kuendelea kujengeana uwezo.