Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

HOSPITALI YA TAIFA YA MAMA NA MTOTO KUJENGWA DODOMA – WAZIRI UMMY MWALIMU

Posted on: August 13th, 2022

Na Englibert Kayombo, WAF – Dodoma.

Serikali kuanza ujenzi wa Hospitali kubwa ya Taifa ya Mama na Mtoto Jijini Dodoma ikiwa ni juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuboresha huduma za Mama na Mtoto na kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya Mhe. @UmmyMwalimu alipopata nafasi ya kuzungumza na wananchi wa Mpunguzi Dodoma leo kwenye Ziara ya Rais wa Jamhuri ya Mujngano wa Tanzania Mhe @samia_suluhu_hassan akitokea Mkoa wa Iringa.

“Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan anakwenda kujenga Hospitali kubwa ya Kitaifa ya Mama na Mtoto katika Jiji la Dodoma, nani kama Samia Suluhu Hassan” amesema Waziri Ummy Mwalimu.

Waziri Ummy amesema Serikali tayari imefanya uwekezaji mkubwa katika miundombinu ya kutolea huduma za mama na mtoto nchini ambapo baadhi ya miradi kama hiyo tayari Rais Samia ameshaitembelea ikiwemo Jengo la Huduma ya Mama na Mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya lililogharimu Shilingi Bilioni 11, pamoja na ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe ambayo imegharimu Shilingi Bilioni 27 ambapo Rais Samia alitembelea Jengo la Mama na Mtoto huku huduma kama hizo zikiendelea kutolewa nchini kote.

Mwisho