Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

HOSPITALI 66 ZIMEANZISHA WODI MAALUM ZA UANGALIZI KWA WATOTO WACHANGA MWAKA 2023/24.

Posted on: May 14th, 2024

UTEKELEZAJI WA BAJETI YA WIZARA YA AFYA 2023/24.


Na WAF - Dodoma

Katika utekelezaji wa huduma za afya kwa watoto wachanga kwa mwaka wa fedha 2023/24 Hospitali 66 zimeanzisha wodi maalum za uangalizi kwa watoto wachanga ambazo zimefanya NCU kufikia 241 nchini.

Waziri wa Afya Mheshimiwa Ummy Mwalimu amesema hayo Bungeni Mei 13, 2024 akiwa anawasilisha hotuba yake ya bajeti ya Wizara ya Afya kwa mwaka wa fedha 2024/25 akielezea utekelezaji wa majukumu ya Wizara katika utoaji wa huduma za Kinga nchini.

"Ongezeko la wodi maalum za uangalizi kwa watoto wachanga (NCU) kumesaidia kuongeza upatikanaji wa NCU nchini kutoka Hospitali 175 mwezi Julai, 2023 hadi kufikia NCU 241 mwezi Machi, 2024." Amesema Waziri Ummy

Aidha, Waziri Ummy amesema kati ya NCU hizo, NCU 156 ziko kwenye Hospitali zinazomilikiwa na Serikali na 85 zipo kwenye Hospitali zinazomilikiwa na Mashirika ya dini na Binafsi.

"Serikali imekarabati NCU kwenye Hospitali 31 ambazo ni Hospitali za Rufaa za Mikoa Sita na Hospitali za Halmashauri 25 katika Mikoa 15 ikiwemo Mkoa wa Singida, Shinyanga, Simiyu, Mara, Geita, Kagera, Mwanza, Manyara, Arusha, Tanga, Songwe, Mbeya, Mtwara, Dodoma na Morogoro.

Mwisho, Waziri @ummymwalimu amesema lengo ni kufikia asilimia 80 ya Hospitali za Halmashauri zote ziwe na NCU ifikapo mwaka 2025 ili kurahisisha utolewaji wa huduma za afya kwa watoto wachanga.