DKT. SHEKALAGHE, AHIMIZA UMOJA, MSHIKAMANO KAZINI KWA WATUMISHI WIZARA YA AFYA
Posted on: September 26th, 2025
Na WAF-Dodoma
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Seif Shekalaghe, amewahimiza watumishi wa wizara hiyo kuimarisha umoja na mshikamano miongoni mwao, ili kuleta tija na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma bora za afya kwa wananchi.
Akizungumza katika kikao maalum na watumishi wizara, leo Septemba 25, 2025 Mtumba jijini Dodoma, Katibu Mkuu Dkt. Shekalange, amesema mshikamano kazini ni nguzo muhimu inayowezesha utoaji wa huduma zenye tija kwa wananchi, huku akihimiza kila mtumishi anapaswa kutimiza wajibu wake kwa weledi, nidhamu na maarifa ili kufikia malengo ya wizara.
“Katika utendaji wetu hakuna kada iliyo muhimu kuliko nyingine, leo hii mtu wa masjala asipo sogeza jalada kwa wakati anaweza kuchelewesha huduma kwa mtu aliyepaswa kupewa rufaa kwenda kwenye matibabu, hivyo hata hawa wenzetu wa masjala nao ni matabibu, lakini pia kwa dereva hivyo hivyo na hata kwa mhudumu anayetayarisha chai ya Ofisi, ni rai yangu tuishi kwa kuheshimiana kil mmoja wetu kwa nafasi yake.” amesema Dkt. Shekalaghe
Dkt. Shekalange ametumia fursa hiyo kutoa shukrani kwa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutoa fedha zilizowezesha kukamilika kwa jengo jipya la Wizara ya Afya na kuanza kutumika, huku likitarajiwa kukabidhiwa rasmi mwezi Oktoba mwaka huu.
“Wengi mnafahamu kuhamia haikuwa kazi rahisi kwani sisi tulikuwa asilimia 96, tukafanya maamuzi magumu ya kuhamia, ile hali ya kutanyuka kwa ofisi ilikuwa inaturudisha nyuma umoja wetu, lakini sasa tunajuana kwa sababu tupo eneo moja. Hizi ni jitihada za Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha na jengo kukamilika,” amesisitiza Dkt.Shekalange.
Aidha, amewataka watumishi kutoa huduma kwa upole na heshima kwa wananchi, kushirikiana wakati wa matatizo, kusaidiana katika changamoto na kuongeza upendo kazini kwa maendeleo ya Pamoja, huku akiwasihi wakurugenzi kuwa karibu na watumishi wao, kusikiliza changamoto zao na kuweka mazingira rafiki ya kazi ili kuongeza tija na morali.
Pia, Dkt. Shekalange amewataka watumishi wote kutunza miundombinu ya jengo jipya la wizara