Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

BURKINAFASO, TANZANIA KUIMARISHA USHIRIKIANO KATIKA HUDUMA YA SARATANI, HUDUMA NYINGINE ZA KIAFYA

Posted on: May 22nd, 2025

Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) Mei 22, 2025 imetembelewa na Mratibu wa Kitaifa wa Mpango wa Afya wa Rais wa Burkina Faso Dkt. Idrissa Traoré, pamoja na ujumbe wake kwa lengo la kuimarisha ushirikiano katika huduma za saratani.


 Ziara hii ni matokeo ya maono  ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt Jakaya Kikwete, wakati wa ujumbe wake wa kidiplomasia nchini Burkina Faso hivi karibuni.


Mkurugenzi Mtendaji wa ORCI, Dkt. Diwani Msemo na timu ya usimamizi, wameonesha hatua za Tanzania katika kushirikiana kwenye kutoa huduma za saratani na nchi hiyo na kusisitiza ushirikiano huo utajikita katika malengo ya pamoja ya uhuru wa afya na matibabu yanayokwenda kufikiwa baina ya mataifa hayo mawili.