Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

BMH YAANZA KAMBI YA UPASUAJI WA MOYO LEO

Posted on: February 14th, 2024



Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) ya jijini Dodoma imeanza kambi ya upasuaji wa moyo kwa watu wazima.

Daktari Bingwa wa Moyo wa BMH, Dkt Kelvin Masava, amesema leo kuwa kambi hii ya pamoja ya wiki moja kati ya wataalam wa BMH na wenzao kutoka Uholanzi itahusisha vipimo na matibabu kwa njia ya upasuaji wa kufungua kifua.

“Mpaka sasa, tuna wagonjwa 450 ambao watafanyiwa uchunguzi, watakaokutwa na matatizo watapatiwa matibabu,” amesema Daktari huyo Bingwa wa Moyo na kufikia sasa wamewafanyia uchunguzi wagonjwa 146 na wagonjwa wawili wamenufaika na huduma ya upasuaji wa kupandikiza mishipa ya damu kwenye moyo kwa mishipa iliyoziba bila kuusimamisha moyo “Off-pump Coronary Artery Bypass surgery”

Dkt Masava ametoa wito kwa watu wazima wenye matatizo ya moyo katika Kanda ya Kati na mikoa ya jirani waitumie kambi hii ya matibabu katika BMH kwa ajili ya kupata suluhisho.

Dkt Masava ameongeza kuwa lengo la kambi hii ya pamoja na wenzao wa Uholanzi ni kutoa huduma pamoja na kubadilishana uzoefu.