BARAZA LA KUTOKOMEZA MALARIA LAJIPANGA KIKAMILIFU KUTOKOMEZA MALARIA NCHINI
Posted on: June 26th, 2023
Na. WAF – Dar Es Salaam
Baraza la Kutokomeza Malaria Tanzania limekaa kikao cha kwanza na kujadili mikakati madhubuti ya utekelezaji wa majukumu yake katika kutokomozea malaria ifikapo 2030.
Kikao hicho kimefanyika leo Jijini Dar Es Salaam, kikiongozwa na Mwenyekiti wa Baraza hilo Leodiger Tenga ambaye amesema kuwa kikao hicho kinalenga kujadili majukumu yao madhubuti kwa kuhakikisha wanafanya kazi walopewa ili kuleta tija na matokeo chanya katika jamii.
“Tumekutana kukumbushana wajibu wetu nini, kuelimishana juu ya hatua zinazochukuliwa na serikali katika mapambano dhidi ya malaria”, ameeleza Mwenyekiti Tenga
Amesema kuwa wao kama baraza watahakikisha wanashirikiana na serikali katika kutekeleza majukumu yao kikamilifu ili kutokomeza Malaria nchini ifikapo 2030
Mwisho, Ikumbukwe Baraza hili lilizinduliwa rasmi tarehe 25 Aprili, mwaka huu na Waziri Mkuu wa Tanzania mara baada ya uteuzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Aidha Wajumbe wamepokea taarifa kutoka mpango wa kutokomeza Malaria NMCP khsu changamoto zinazokabili utekeleezaji wa afua mbali mbali za kutokomeza Malaria pamoja na upungufu wa bajeti y utekelezaji wa mpango mkakati ili kutokomeza Malaria nchini kufikia mwaka 2030, katika michango yao wajumbe wameonyesha ari ya kiwango cha juu katika kushirikisha sekta zote mtambuka nchini katika kufanikisha kufikiwa kwa malengo ya serikali.