ASILIMIA 98 YA WAJAWAZITO MKOANI LINDI HUJIFUNGULIA KATIKA VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA.
Posted on: September 9th, 2025
Na WAF – Lindi
Asilimia 98 ya akinamama wajawazito mkoani Lindi hujifungulia katika vituo vya kutolea huduma za afya hali ambayo imechagizwa na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali katika kuboresha miundombinu na kuongeza rasilimali watu.
Taarifa hii imebainika Septemba 8, 2025, mkoani Lindi, wakati wa ziara ya Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Grace Magembe, iliyoangazia usimamizi shirikishi na kukagua ubora wa huduma katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi – Sokoine.
“Tulipotoka ilikuwa tofauti kabisa, huduma hazikuwa na ufanisi pia idadi ya wajawazito waliokuwa wakijifungulia vituoni haikufikia hata asilimia 40. Wengi walilazimika kutegemea wakunga wa jadi kutokana na uhaba wa vituo. Leo hii tumefikia 98%, jambo linalothibitisha jinsi huduma zilivyoboreshwa,” alisema Dkt. Magembe.
Amesema uwekezaji huo umeongeza tija siyo tu katika huduma za mama na mtoto, bali pia katika huduma nyinginezo ngazi zote za afya.
“Zamani hakukuwa na ‘shift’, wahudumu walikuwa wachache. Hivi sasa Serikali imeajiri watoa huduma wa kutosha, tunapata zamu mbili hadi tatu, jambo linaloongeza ufanisi,” ameongeza Dkt. Magembe.
Aidha, Dkt. Magembe amewasisitiza watumishi wa sekta ya afya kujenga mshikamano, kupendana na kusaidiana katika utekelezaji wa majukumu yao, akibainisha kuwa kila mmoja ana mchango katika kulijenga taifa lenye huduma bora za afya.
Pia amewataka kuzingatia maadili ya utumishi wa umma ili thamani ya miradi na uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan iendelee kudumu.
Akiwa hospitalini hapo, Dkt. Magembe ametembelea wodi ya wanaume, bohari ya dawa na kupongeza uongozi wa hospitali kwa kuhakikisha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba umeimarika. Pia alikagua jengo la mtambo wa kuchakata hewa tiba ya oksijeni na kuahidi kulifanyia kazi ili uchakataji uanze haraka na kupunguza gharama za kununua mitungi ya gesi kutoka maeneo ya mbali.
Kwa upande wake, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Lindi – Sokoine, Dkt. Alexandre Makalla, ameshukuru kwa ujio wa Dkt. Magembe, akieleza kuwa changamoto ndogo ndogo zilizopo zi