KAMATI YA BUNGE YAIPONGEZA SERIKALI KWA KUTAMBUA NA KUYAPA KIPAUMBELE MAGONJWA ADIMU
Posted on: August 14th, 2026Na Shaban Juma, Dodoma
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI imeipongeza Serikali kwa hatua ya kutambua na kuendelea kutoa kipaumbele katika kukabiliana na magonjwa adimu nchini, huku ikisisitiza umuhimu wa kuimarisha uwekezaji katika huduma, utafiti na elimu kwa jamii kuhusu magonjwa hayo.
Akizungumza leo Agosti 13, 2026, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Dkt. Johannes Lukumay, amesema hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kutambua magonjwa adimu ni muhimu katika kuhakikisha wananchi wanaoishi na magonjwa hayo wanapata huduma stahiki licha ya kuwa idadi yao ni ndogo.
Kupitia taarifa iliyowasilishwa mbele ya Kamati na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Florence Samizi, kwa niaba ya Waziri wa Afya, Mhe. Mohamed Mchengerwa, Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali katika kuimarisha huduma za magonjwa adimu, ikiwemo kuandaa sera na miongozo, kuimarisha upatikanaji wa dawa, kutoa elimu kwa jamii, kuboresha huduma za uchunguzi na matibabu pamoja na kuimarisha tafiti.
Dkt. Lukumay pia amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa jitihada za kuhakikisha magonjwa adimu yanatambuliwa na kupewa nafasi katika ajenda ya afya nchini, akisema uongozi wake umeendelea kusukuma mbele juhudi za kuimarisha huduma kwa watu wanaoishi na magonjwa hayo. Taarifa ya Wizara inaeleza kuwa mabadiliko makubwa katika utekelezaji wa mikakati yalifanyika chini ya uongozi wa Rais Samia, ikiwemo kuzinduliwa kwa kampeni ya kitaifa ya magonjwa adimu mwaka 2021 na maelekezo ya kuyapa kipaumbele.
Aidha, Kamati imeshauri kuongezwa kwa bajeti kwa ajili ya kukabiliana na magonjwa adimu, hususan katika maeneo ya utafiti, elimu kwa jamii, utambuzi wa mapema na uendelezaji wa wataalamu, ili kuongeza uelewa kuhusu magonjwa hayo na kuondoa dhana potofu zinazoweza kuwafanya wagonjwa kuonekana kama wameathiriwa na imani za kishirikina badala ya kutambuliwa kuwa wanahitaji huduma za afya.
Taarifa ya Wizara imebainisha kuwa uelewa mdogo wa jamii ni miongoni mwa changamoto zinazokabili huduma za magonjwa adimu, hali inayochangia unyanyapaa kwa wagonjwa na familia zao. Serika