Customer Feedback Centre

Ministry of Health

ZINGATIENI AFUA ZA LISHE ILI KUWA NA JAMII YENYE AFYA BORA

Posted on: September 26th, 2023

Na. WAF - Dodoma


Wizara ya Afya kupitia idara ya Sera na Mipango imeanza kutekeleza agizo la Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan la kufanya mapitio ya Sera ya chakula na lishe ya Taifa ya Mwaka 1992 ili iendane na wakati kwa kuwa jamii yenye Afya bora ni vyema kuzingatia afua za lishe.


Hayo yamesemwa leo Septemba 26, 2023 na Mchumi Mkuu kutoka Idara ya Sera na Mipango Wizara ya Afya Bw. Mintanga Milulu wakati wa kikao kazi cha kufanya mapitio ya hayo ya Sera ya chakula na lishe ya Taifa ya Mwaka 1992.


“Tumeanza kupitia Sera hii ya chakula na lishe ya Mwaka 1992 ili iendane na wakati kama alivyoagiza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na iweze kutekelezwa kama ambavyo inastahili kwa kulete tija ambayo imekusudiwa katika kujenga Afya bora kwa Watanzania”. Amesema Bw. Milulu


Aidha, Bw. Milulu amesema Dira ya Sera ya Afya ya Mwaka 2007 inasema “tunataka kuona Jamii yenye Afya bora na ustawi ambayo itachangia kikamilifu katika ukuaji wa uchumi wa Taifa pamoja na mtu binafisi”.


“Sera hii inamgusa mwananchi kwa sababu ni swala la Lishe na swala hili ni swala mtambuka ambalo linamgusa mtu mzima, kijana hata mtoto hivyo katika kujenga jamii yenye Afya bora ni vyema tukazingatia afua ya lishe”. Amesema Bw. Milulu


Amesema, Sera hiyo ya chakula na lishe itazingatia Dira ya Afya ambayo itapelekea ukuaji wa uchumi wa mtu mmoja mmoja, Jamii pamoja na Taifa kwa ujumla kama ilivyoelekezwa kwenye Sera ya Taifa ya Mwaka 2007


Hata hivyo, Bw. Milulu amesema katika kikao hicho wamekutana na wadau wote wanaotoka katika Sekta mtambuka zinazotekeleza masuala ya lishe, wadau wamaendeleo pamoja na Sekta bimafsi.


“Hivyo katika hatua hii ya awali ya kutekeleza maelekezo haya tutatoka na rasimu ambayo itakuwa yenye tija na kujumuisha maoni ya wadau wote muhimu katika kutekeleza swala hili la kupitia upya Sera ya chakula na lishe”. Amesema Bw. Milulu