Ministry of Health

WAZIRI MCHENGERWA AZINDUA BODI MPYA BENJAMIN MKPA, ASISITIZA MIRADI YA KIMKAKATI, HUDUMA BORA ZA AFYA

Posted on: April 23rd, 2026

Na Atley Kuni, WAF-Dodoma

Bodi mpya ya Wadhamini wa Hospitali ya Benjamin Mkapa imezinduliwa rasmi, huku viongozi wakisisitiza kukamilisha miradi iliyoanzishwa na kuongeza ubunifu wa huduma mpya zitakazogusa moja kwa moja mahitaji ya jamii.

Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Afya Mhe Mohamed Mchengerwa Aprili 22, 2026 jijini Dodoma wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo iliyofanyika hospitalini hapo na kukabidhiwa nyezo za utendaji kazi.

"Bodi iliyopita imeacha alama muhimu tangu hospitali ilipoanza kutoa huduma rasmi, ikisimamia utekelezaji wa miradi kadhaa ikiwemo uzalishaji wa hewa tiba ya oksijeni, uanzishwaji wa chuo cha afya na sayansi shirikishi, pamoja na kuendeleza ujenzi wa jengo la matibabu ya saratani uliokwisha kufikia asilimia 68" amesema Mchengerwa.

Waziri Mchengerwa amesema mafanikio mengine yaliyopatikana ni pamoja na maandalizi ya huduma za upandikizaji figo, uanzishaji wa huduma saidizi ya uzazi (AIVF), ukarabati wa vyumba vya upasuaji, pamoja na kuboreshwa kwa makazi ya watumishi wa afya hatua zinazolenga kuongeza ubora wa huduma na upatikanaji wake kwa haraka zaidi.

Katika kuhakikisha ufanisi wa uongozi, Serikali imeahidi kushughulikia haraka upungufu wa mjumbe mmoja wa Bodi, huku ikisisitiza ushirikiano wa karibu kati ya Wizara na uongozi wa hospitali ili kuharakisha maendeleo ya sekta ya afya.

Waziri Mchengerwa amefafanua kuwa Uzinduzi huo unatazamwa kama hatua mpya ya mageuzi katika utoaji wa huduma za afya, ukilenga kuinua viwango vya matibabu na kuimarisha matumaini ya wananchi kupata huduma bora, za kisasa na zinazopatikana kwa wakati.

Awali akimkaribisha Waziri kuongea katika hafla hiyo, Mwenyekiti wa Bodi Prof. Edward Hosseah amesema anamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini huku akiahidi kutumia maarifa aliyonayo kuushauri uongozi wa hospitali kwa weledi.

"Mhe. Waziri tunaomba utufikishe Salaam zetu kwa Mheshimiwa Rais, lakini kwa niaba ya Wajumbe uliowateuwa tunakuahidi tutasimamia na kumshauri Mkurugenzi na wasaidizi wake kwa kutumia taaluma zetu kwenye eneo la Tiba na