Ministry of Health

WAZIRI MCHENGERWA AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA WHA79

Posted on: May 18th, 2026

Na John Mapepele

Geneva, Uswisi

Waziri wa Afya Nchini, Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa ameongoza ujumbe wa Serikali ya Tanzania katika ufunguzi rasmi wa Mkutano Mkuu wa 79 wa Shirika la Afya Duniani (WHA79) ulioanza leo Mei 18, 2026 mjini Geneva, Uswisi.

Mkutano huo mkubwa duniani katika sekta ya afya unashirikisha zaidi ya nchi 180 katika maeneo mbalimbali ulimwenguni, Mkutano umefunguliwa na
Tedros Adhanom Ghebreyesus, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO).

"Mkutano wa 79 wa Baraza la Afya Duniani (WHA79) unafanyika kuanzia tarehe 18 hadi 23 Mei 2026 mjini Geneva, Uswisi.mkutani huo unawakutanisha wajumbe kutoka Nchi Wanachama wa WHO kwa lengo la kushughulikia shinikizo kubwa linaloikabili mifumo ya afya na kuweka sera za afya za Kimataifa, huku ukisisitiza huduma ya afya kwa wote, afya ya akili na athari za mabadiliko ya tabianchi kwa afya." Amefafanua Mheshimiwa Mchengerwa

Kwa mujibu wa Mheshimiwa Mchengerwa, maeneo makuu ya mjadala katika mkutano wa mwaka 2026 ni pamoja na:Huduma ya Afya kwa Wote (UHC) na Ufadhili ambapo amesema Nchi wanachama na mashirika ya kiraia wanatoa kipaumbele kwa kuharakisha mifumo ya ufadhili wa afya inayoongozwa na nchi husika, mageuzi ya kidijitali katika mifumo ya afya, na kuhakikisha ushiriki wa kijamii ili kuimarisha mamlaka ya afya ya Kitaifa.

Aidha, amesisitiza eneo lingine linalopewa mkazo ni Afya ya Akili ambapo amesema kufuatia Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Umoja wa Mataifa wa mwaka 2025 kuhusu Magonjwa Yasiyoambukiza (NCDs) na afya ya akili, WHA79 ina kampeni kubwa za utetezi na matukio maalum yanayolenga kutafsiri ahadi za kimataifa kuwa mikakati halisi ya kitaifa ya afya ya akili.

Ameeleza kuwa,Jambo lingine litakalojadiliwa ni Tabianchi na Afya ambapo amefafanua kuwa ingawa si ajenda maalum ya pekee, athari zinazoendelea za mzozo wa tabianchi na matumizi ya mafuta ya kisukuku ni sehemu muhimu ya mijadala inayohusu afya ya