Customer Feedback Centre

Ministry of Health

WAUGUZI, WAKUNGA WABEBA ASILIMIA 60 WATUMISHI SEKTA YA AFYA

Posted on: March 18th, 2024


Na WAF, Dodoma

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema asilimia 60 ya watumishi katika sekta ya afya nchini ni wanatoka kada za uuguzi na ukunga hivyo kuchangia ubora wa huduma zinazotolewa katika Hospitali na Vituo vya kutolea huduma za afya.

Moleli amebainisha hayo Machi 18, 2024 wakati wa kikao kazi cha kufanya tathimini ya utekelezaji wa utendaji kazi wa utoaji wa huduma za uuguzi na Ukuguzizoezi lililoenda sambamba na uzinduzi wa jarida la idara ya Uuguzi na Ukunga jijini Dodoma.

Dkt. Mollel amesema kada ya Uuguzi imekuwa muhimu katika kutoa huduma bora kwa sababu asilimia 80 ya kazi zinatekelezwa na kada hiyo na kutoa rai kada hiyo kujumuishwa kwenye mfumo wa utoaji wa maamuzi

“Ukiona kituo cha afya kinatoa huduna bora ni kwa sababu ya uwepo wa wauguzi ambao ndio wamekuwa watendaji wakuu ambao wanakaa muda mwingi na wagonjwa hivyo ni muhimu wakawekwe kwenye mfumo wa uongozi na utoaji wa maamuzi na uundwaji wa sera”

Dkt. Mollel Ametoa wito kwa wauguzi na wakunga wanapopata fursa ya kuingia ndani ya mfumo wa uongozi kuhakikisha mambo yanaboresha sekta ya Afya lakini pia maslahi yao.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa idara ya Huduma za Uuguzi na Ukunga Bi. Ziada Sella ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kuajiri Wauguzi na Wakunga zaidi ya elfu arobaini kwa kipindi cha mwaka 2022/2023 na kuongeza kuwa kada hiyo inadhamana kubwa katika utoaji wa huduma hivyo wazingatie miongozo, kanuni na sheria zilizowekwa kwa maslahi ya taifa.

“tunamshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa kibali cha kuajiri wauguzi na wakunga zaidi ya elfu arobaini hii inaonyesha umuhimu na dhamana ya kada hii kwa sababu hawa ndio hutumia muda mwingi kukaa na wagonjwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi msaidizi wa Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe TAMISEMI Dkt. Paul Chawote amesema TAMISEMI itaendelea kupokea maelekezo ya wizara ya Afya na kushirikiana na Halmashauri na Mikoa kuhakikisha utoaji wa Huduma za afya ngazi za msingi zinaimarishwa.



Kikao hichon kilicho wakutanisha Viongozi wauguzi na Ukunga kote nchini kimeenda na kauli Mbiu isemayo “Huduma Staha na Mawasiliano ni Wajibu wa Kila Mtoa Huduma za Afya”.


MWISHO