Customer Feedback Centre

Ministry of Health

WATUMISHI WA SEKTA YA AFYA WATAKIWA KUBORESHA MAWASILIANO BAINA YAO NA WAGONJWA KULETA UBORA WA HUDUMA

Posted on: April 22nd, 2024


Na WAF - Arusha

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. John Jingu, amewataka watumishi wa sekta ya afya kuongeza kuimarishaji wa mawasiliano kati yao na wagonjwa ili kuboresha huduma za afya nchini.

Dkt. Jingu ametoa kauli hiyo leo, Aprili 22, 2024 wakati wa kikao na watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha, Mount Meru, baada ya kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje lenye ghorofa nne.

Akizungumza, Dkt. Jingu amesisitiza umuhimu wa mawasiliano katika utoaji wa huduma za afya kwani mawasiliano bora yatasaidia kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi na kuhakikisha majibu yanatolewa kwa haraka na ufanisi.

"Kudumisha mawasiliano kati yetu sisi watumishi na wananchi, ambao ni wateja wetu, ni jambo la msingi sana katika kuboresha huduma za afya, hivyo tuzingatie lugha za staha na zenye maadili katika mawasiliano yetu ili tuendelee kufanya kazi kwa weledi mkubwa," ameongeza Dkt. Jingu.

Aidha, Dkt. Jingu ameeleza umuhimu wa kuimarisha miundombinu ya huduma za afya kwakuwa serikali ina jukumu la kuhakikisha inaboresha na kujenga majengo yenye hadhi na kutoa huduma bora kwa wananchi.

Aidha amesema uimarishaji wa miundombinu na huduma bora utarahisisha Hospitali ya Mount Meru kuwa kituo cha umahiri katika utoaji wa huduma za afya, kwa kuwa na watendaji wenye ari na kufanya uwekezaji katika miundombinu.

Awali, akitoa taarifa yay a maendeleo ya Hospitali hiyo Kaimu mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mount Meru Dkt. Kipapi Mlambo amesema kuwa Hospitali hiyo imekua ni kiungo muhimu katika mkoa wa Arusha kwakuwa na huduma rafiki na hivyo kuendelea kuboresha miundombinu mbalimbali Pamoja na kujenga jengo la watu muhimu kwakua hospital hiyo iko katika mkoa wa kimataifa