Customer Feedback Centre

Ministry of Health

WANANCHI WATAKIWA KUPIMA AFYA ZAO KABLA YA KUANZA KUFANYA MAZOEZI.

Posted on: August 10th, 2023

Na: Shaban Juma, Dodoma

Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Mohamed Y. Janabi amewataka Wananchi kupima afya zao kabla ya kufanya mazoezi ili kusaidia katika kuboresha afya na kinga ya mwili.

Prof. Janab ameyasema hayo leo Agosti 10,2023 Jijini Dodoma wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu taarifa utekelezaji wa shughuli mbalimbali na mwelekeo wa mwaka wa fedha 2023/24

Aidha Prof. Janabi amesema kuwa kupima afya kunasaidia kujua uwezo wa mwili katika kukabiliana na mazoezi ambayo hufanywa kama vile mpira na kukimbia.

Hata hivyo Prof. Janabi amesema kuwa katika kukabiliana na maradhi mbali mbali ikiwemo tatizo la moyo ni vyema kwa wananchi kupima mara kwa mara afya zao kwani baadhi ya magonjwa ni ya ghafla ambayo husababisha kupoteza Maisha.

“Mazoezi ni kitu kizuri ila kapimeni afya zenu kabla ya kuanza hii itawasaidia katika kuimarisha afya na kujiepusha na magonjwa ambayo yanaweza kuepukika” Amesema Prof Janabi.